Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chertered, Sanjay Rughani amesema benki itaendelea kuwaelimisha watu katika mataifa mbalimbali juu fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania.
Sanjay alitoa kauli wakati wa hafla ya kusherehekea mwaka mpya wa China uliondaliwa na benki hiyo na kuhudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba.
Amesema benki hiyo ina matawi mengi katika mataifa mbalimbali hivyo itatumia mwaya huo kutoa elimu kwa wateja wake juu ya umuhimu wa kuwekeza Tanzania.
“Inabidi tuwaelimishe watu wa China na mataifa mengine ambako benki hii ipo juu ya fursa zilizopo Tanzania na malighafi za kutosha zinazochechea uwekezajia,” amesema Rughani.
Amesema nia ya Serikali ni kuimarisha uchumi wa Tanzania hivyo wataangalia sheria zinazozenga nchi hasa nyanza za kukuza uchumi ili wajue namna gani wataweza kusaidia.
No comments
Post a Comment