Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, July 4, 2015

Maaskofu na Masheikh, waonya CCM

BAADHI ya viongozi wa madhehebu ya kidini nchini, wameapa kutomuunga mkono mgombea yeyote wa urais anayetafuta urais kwa hongo, hata kama anang’aa kama jua wakati wa mchana na mwezi nyakati za usiku. Maaskofu na Masheikh walitoa kauli hiyo, walikuwa kwenye kongamano la kidini, lililohudhuriwa na viongozi wa madhehebu ya kidini takribani 460, wakiwamo maaskofu, mashekhe na wachungaji. Viongozi walioshiriki kongamano hilo, ni kutoka mikoa ya Morogoro, Dar es Salaam, Kagera, Katavi, Tanga, Mara, Mwanza, Iringa, Njombe, Rukwa, Mbeya, Singida, Dodoma, Ruvuma, Tabora, Unguja, Kilimanjaro, Arusha, Lindi na Mtwara. Mkumbaru alisema iwapo nchi itaongozwa na mtu anayenunua uongozi atagawa utajiri wa taifa nje, ambapo kwa kipindi hiki Tanzania inataka rais wa kuliponya taifa ambalo kwa kuwa lipo mahututi kwa madeni na rushwa. Alisema ni wakati muafaka vijana kote nchini kujithamini na kuacha kutumika kama madaraja ya kuvushia wenye tamaa ya madaraka. Alisema wengi wanaowania madaraka, wakimaliza kutimiza kile wanachokitafuta, hawaonekani tena. Alisema, “Ni vema mwaka huu vijana waonesheni okomavu wa kusimamia uwezo wa mtu na siyo chama au dhehebu lake. Nchi hii inahitaji mabadiliko na sio wataka urais kwa rushwa.” Sheikh Mkambaru hakumtaja anayesema, “mwanasiasa anayetafuta urais kwa njia ya rushwa.” Hata hivyo, anayetuhumiwa kugawa fedha ili kupata madaraka, ni pamoja na Edward Lowassa, Bernard Membe, Mwigulu Nchemba, Mizengo Pinda na January Makamba. Alisema kama watanzania hawatakuwa makini na kuzikataa rushwa, watalikabidhi taifa kwa vigogo wa mihadarati, wauaji wa albino na mafisadi na kamwe nchi yetu haitainuka kiuchumi. Alisema pamoja na Tanzania kugundua gesi nyingi, mafuta na madini mengine yanayogunduliwa kila kukicha, bado matumizi yake hayajazingatia usawa; badala yake, gesi na mafuta hayo yananufaisha kikundi kidogo cha watu. Mwenyekiti wa kamati hiyo, Askofu William Mwamalanga, amevionya vyama vya siasa kuacha mara moja kuwapeleka wagombea wa urais kwenye kaburi la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ili kuhiji wakati kiuhalisia hawana maadili ya mwasisi huyo. Mwamalanga aliwataka watia nia hao wamkimbilie Mungu na kutubu kwake kwani yeye ndiye mwenye msamaha kwa kila mwanadamu na siyo Mwalimu Nyerere. “Kila mtu hapa ana chama chake cha siasa kama yalivyo madhehebu yetu ya kidini, ambapo kila mtu anasema dini yake ni bora kuliko ya mwenzake. “Je, umasikini, njaa, rushwa, madhara ya mihadarati na uchafu mwingine ndani ya taifa vimechagua dini, au chama? Mwaka huu ni mwaka wa kupata kiongozi mwenye huruma na wannachi; siyo kiongozi anayejitaza yeye binafsi,” ameeleza. Wakisoma tamko la vijana mbele ya maaskofu na mashekhe wanaohudhuria kongamano hilo baadhi vijana waliomaliza vyuo vikuu vya Sua, UDOM, UDSM, Tumaini, Teofilo Kisanji, Saut na Mzumbe, wamekiri kutokuwa na mchango wowote wa kukuza uchumi wa nchi, kupitia sekta za kilimo na elimu. Vijana hao walitaja sifa tisa ambazo sharti anayetaka kuwa rais wa awamu ya tano, ni lazima awe nazo. Sifa hizo, ni pamoja na kuwa na uwezo wa kuwaondolea wananchi kwenye mfumo kandamizi na awe hajawahi kukataliwa au kuonywa na viongozi wa nchi au shutuma zozote. Walitaka mhusika kutojilimbikizia utajiri, kashfa za rushwa, mpenda haki, mwenye uwezo wa kuongoza, mkweli; hajawahi kutorosha fedha nje ya nchi na hajaonekana kwa wapiga ramli ili kutafuta kupendwa na watanzania. Baada ya mafunzo hayo, vijana waliamriwa kwenda kote nchini kuelimisha wananchi sifa za Rais ajaye ili kuleta mabadiliko ya kweli kwa taifa na vizazi vijavyo. Alitangaza mwaka 2015 kuwa ni mwaka wa mabadiliko ya kweli kifikira kwa kuwakata watoa rushwa hadharani ili haki iwe wimbo kwa kila mtanzania.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment