Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, June 27, 2015

Serikali yakubali yaishe, kutojadili muswada wa habari

Dodoma. Ni rasmi sasa Serikali imekubali yaishe kwa kuundoa muswada wa Sheria ya Upatikanaji Habari 2015 hadi Bunge lijalo ili uweze kuboreshwa na kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza hapo baadaye katika jamii. Hatua hiyo ya Serikali imekuja baada ya kuwapo mashinikizo ya muda mrefu kutoka kwa wadau wa habari wakilalamikia uharaka wa kuipitisha sheria hiyo bila kuwashirikisha tangu muswada ulipoletwa bungeni awali Machi mwaka huu. Akiwasilisha taarifa fupi ya Serikali bungeni jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandyosa alisema, Kamati ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii imeomba uahirishwe ili ipate fursa zaidi ya kupokea maoni ya wadau na kuandaa muswada bora kwa masilahi ya Taifa. Alisema kamati hiyo ilikaa Juni 22 na kujadili kwa kina maoni ya wadau na kushauri kuwa,inataka muda zaidi wa kuujadili. “Serikali imetafakari maoni ya kamati na kuafiki muswada uendele kufanyiwa kazi hadi hapo itakapokuwa imekamilisha kazi ipasavyo na kuwasilisha bungeni.” Aliongeza: “Matarajio ni kwamba muswada huu utasomwa kwa mara ya pili na ya tatu katika Bunge lijalo…naomba kutoa ushauri kwa wadau wanaoendelea kutoa ushauri na ambao bado wanaendelea kufanya hivyo ili tuweze kupata muswada na sheria iliyo bora kwa manufaa ya jamii na masilahi ya Taifa,” alisema na kuondoka kwenda kurudisha fomu za udhamini wa kuwania urais CCM . Hata hivyo, Profesa Mwandyosa alisema, pamoja na kuahirisha muswada huo hadi Bunge la 11, bado Serikali haioni kuwa ulikuwa wa dharura kama wengine wanavyodai kwa kuwa ulichapishwa awali Februari 20 na kusomwa kwa mara ya kwanza katika vikao vya Machi hadi Aprili. Alisema siku zote mchakato wa kutunga sheria nchini ni shirikishi na Serikali inapotunga sheria hizo huangalia manufaa mapana ya jamii na masilahi ya Taifa. Kuondolewa kwa muswada huo uliotakiwa kusomwa leo, katika msululu wa miswada iliyotakiwa kujadiliwa na kupitishwa katika Bunge hili, ni ushindi wa awali kwa wadau mbalimbali wanaotaka Serikali iahirishe shughuli hiyo hadi Bunge lijalo kuzuia kupitishwa na makosa kutokana na ukweli kuwa akili za wabunge zipo majimboni. Kwa majuma kadhaa, viongozi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri (TEF) walionekana ‘wakikesha’ katika viwanja vya Bunge ili kuishawishi Kamati ya Maendeleo ya Jamii na Spika wa Bunge, Anne Makinda wauondoe katika ratiba ya sasa.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment