Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, May 13, 2015

Mwanamke mweusi ndio malkia wa urembo Japan

Ariana Miyamoto aliingia katika shindano la malkia wa urembo nchini Japan baada ya rafikiye mwenye mchanganyiko wa rangi kujiua. Na alivumilia unyanyasaji baada ya kushinda taji hilo kwa sababu ya rangi yake. Licha ya kuzuiwa na rangi yake,Miyamoto aliweza kutumia umaarufu wake kusaidia kupigana dhidi ya ubaguzi kama vile mwanamitindo Naomi Campbell alivyovunja tamaduni katika sekta ya mitindo miaka kadhaa iliopita. ''Nina sumbua sana'', alisema Miyamoto mwenye umri wa miaka 21 aliyezaliwa na mama wa Kijapan na baba mweusi kutoka Marekani.Nilijiandaa kukosolewa''. ''Nitadanganya iwapo nitasema haikuniumiza.Mimi ni raia wa Japan,mimi husimama na kuinamisha kichwa wakati ninapojibu simu.Lakini ukosoaji umenipatia motisha zaidi aliambia AFP katika mahojiano. ''Sikujali shinikizo zozote kwa sababu niliingia katika shindano hilo kutokana na kifo cha rafiki yangu.Lengo langu ilikuwa ni kuwahamasisha watu kuhusu ubaguzi wa rangi'',aliongeza Miyamoto ambaye aliteswa shuleni katika eneo la bandari ya Sasebo karibu na Nagasaki. Mitandao ya kijamii ilitangaza ushindi wa Miyamoto ,huku wengi wakilalamika kwamba ushindi huo ungemwendea raia mwenye mizizi ya Japan na wala sio mtu mwenye rangi.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment