Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, May 13, 2015

Marekani na Urusi wateta juu ya Ukraine

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry,amesema kwamba amekuwa na mazungumzo ya kirafiki kuhusiana na mzozo wa Ukraine pamoja na mambo mengine na mwenyeji wake rais wa Urusi , Vladimir Putin, katika ghuba ya bahari ya shamu pwani ya Sochi. Lakini pia Kerry alikutana na waziri wa masuala ya mambo ya kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov, katika ziara yake ya kwanza tangu mgogoro wa Ukraine ulipoanza mwaka wa jana. Kerry pia hakusita kuzungumzia masuala ya ziada ambayo yalijiri katika mazungumzo yao kwamba ni juu ya yanaoendelea baina ya Iran na Syria. Amesema kwamba ni muhimu kuzingatia makubaliano waliyofikia baina ya Marekani na Urusi wakati wakiangazia masuala mengine yanayo ikabili dunia. Mapema kabla ya kuanza mazungumzo hayo, waziri huyo ma mambo ya nchi za nje wa Marekani, alipata fursa ya kuweka shada la maua katika makaburi ya askari waliopigana vita vikuu vya pili vya dunia mjini Sochi. Uhusiano baina ya Urusi na Marekani umeshuka kwa kasi baada ya Urusi kujihusisha harakati za krimea na kuwaunga mkono wapiganaji wa waasi walioko upande wa Mashariki mwa Ukraine.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment