Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, May 6, 2015

Milipuko yatokea jeshini Sudan.

Kumetokea milipuko katika maeno ya jeshi nje ya mji mkuu wa Sudan, Khartoum. Wakazi katika wa eneo la Omdurman la ukanda wa magharibi wa mto Nile wamesema mapema usiku wa manane walisikia mlipuko wa kwanza na baadae makombora ya kutungulia ndege kutoka upande wa majeshi ya serikali. Msemaji wa serikali ya Sudan amethibitisha askari wake walifanya mashambulizi na kulenga kundi wasilolifahamu lakini akakanusha kikosi chake na vifaa vyao vya kijeshi kushambuliwa. Miaka mitatu iliyopita Sudan iilituhumu Israeli kwa kufanya mashambulizi ya anga kwenye kiwanda cha silaha mjini Khartoum ambapo pia kuna taarifa kuwa ndege za Israel pia zilifanya mashambulizi kwenye misafara ya silaha zilizokuwa zikisafirishwa kwenda Gaza. Israel haijatoa taarifa zozote rasmi kujibu shutuma hizo.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment