Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, May 6, 2015

Khan wa Bollywood kwenda jela miaka 5.

Mwigizaji maarufu wa filamu za Bollywood nchini India Salman Khan amekuhumiwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mtu mmoja asiye na makazi alipokuwa akiendesha gari huku akiwa amelewa mjini Mumbai. Khan alikuwa ameshtakiwa kwa kuua bila kukusudia baada ya kuelekeza gari lake kwenye kundi la watu waliokuwa wamelala kwenye njia kando ya barabara mwaka 2002. Mmoja kati ya watu hao Noor Ullah Khan alikufa katika ajali hiyo. Khan amedai kuwa dereva wake ndiye anayepaswa kulaumiwa lakini mashuhuda wanasema mwigizaji huo ndiye aliyekuwa kwenye usukani na alikimbia baada ya kutokea kwa ajali hiyo. Kwa mujibu wa jaji wa mahakama hiyo mwigizaji huyo anaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment