Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, August 31, 2014

Mawaziri, wabunge kutimuliwa kwenye nyumba TBA Dodoma


 
Na Beatrice Moses, MwananchiDar es Salaam. Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imefanya uamuzi mgumu wa kuwatimua baadhi ya wapangaji wa nyumba zake zilizopo mjini Dodoma ambao ni wadaiwa sugu, wakiwamo mawaziri saba na wabunge 15.
TBA katika kutekeleza uamuzi huo imekabidhi Kampuni ya Yono Action Mart orodha ya majina ya watu hao wanaodaiwa kiasi cha Sh800 milioni, ili waondolewe kwa nguvu kwenye nyumba hizo wanazoishi.
Akizungumza na Mwananchi juzi Mkurugenzi Mtendaji wa TBA, Elius Mwakalinga, alithibitisha kuwa ofisi yake inachukua hatua hiyo kwa mujibu wa sheria kwa sababu wapangaji hao wamekwenda kinyume na mikataba yao.
“ Hatukupenda kuchukua hatua hii, lakini ukweli ni kwamba madeni hayo ni ya muda mrefu, kazi tunayofanya ni kwa manufaa ya maendeleo ya nchi na siyo yetu binafsi, hivyo tulitegemea wangetimiza wajibu wao wa kulipa lakini imekuwa kinyume,” alisema Mwakalinga.
Alisema fedha ambazo TBA inadai hadi sasa zimefikia jumla ya Sh 800 milioni ambazo kama zingekuwa zimelipwa zingewasaidia kutimiza wajibu wao wa kujenga baadhi ya nyumba mpya au kukarabati zile zinazotakiwa kufanyiwa hivyo.
“Walipewa notisi na ofisi yetu kule Dodoma baadhi yao waliitikia wito kwa kulipa madeni yao, wakiwamo hata maofisa wa Ikulu, walitoa ushirikiano mzuri, nafikiri kwa kutambua wajibu tulio nao TBA,” alisema.
Mwakalinga alisema kuwa TBA imeona iwahusishe kampuni ya udalali ya Yono Action Mart kwa sababu wao wana majukumu mengi ya ujenzi wa nyumba mpya za watumishi wa Serikali.
“ Gharama za kumlipa dalali huyo, watatakiwa kulipa hao hao wanaodaiwa kwa mujibu wa sheria, sisi hatuna bajeti hiyo,” alisema Mwakalinga ambaye alikataa kuwataja wadaiwa hao akieleza kuwa jukumu hilo tayari lipo kwa Yono.
Mkurugenzi wa Yono Action Mart, Yono Kevela, kwa upande wake alisema baada ya kupokea kazi hiyo, walitoa notisi ya siku 14 kwa wahusika ili kuwapa nafasi ya kulipa madeni yao.
“ Wale ambao wamelipa kutokana na ile notisi wamejinusuru, lakini wale ambao hawajalipa kwa kweli nimetuma kikosi kazi changu ambacho ninakiamini, kwamba hakina woga katika kutimiza majukumu tuliyopewa, natarajia kesho wataanza kazi, hiyo,” alisema Kevela. Baadhi ya mawaziri waliotajwa kwenye orodha hiyo ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dk Abdallah Kigoda, anayedaiwa Sh7.5 milioni, ambaye alipohojiwa na gazeti hili kwa njia ya simu kuhusu deni hilo alisema: “Mimi sina habari hiyo nipo Nairobi, Kenya,”.
Mwingine ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu anayedaiwa Sh 9.4 milioni, ambaye aliliambia gazeti hili kuwa ana taarifa ya deni hilo, lakini kwa wadhifa wake hawajibiki binafsi.
“ Nakumbuka niliona barua, lakini kwa utaratibu ninaoujua ni kwamba mawaziri wote hatujigharamii kwa hilo , bali tunalipiwa na Serikali sasa nafikiri labda wizara ilijisahau, nakuhakikishia binafsi siwajibiki,” alisema Nyalandu.
Juhudi za gazeti hili kuwasiliana na mawaziri wengine wakiwamo na naibu mawaziri ambao majina tunayo, zilikwama baada ya baadhi yao kushindwa kupatikana ofisini na simu zao kuita bila majibu huku wengine simu hazikupatikana.
Wabunge
Kwa upande wa wabunge ni mbunge wa Bariadi John Cheyo(UDP) ambaye anadaiwa Sh 4.2 milioni, alipohojiwa kuhusu deni hilo alishtuka na kueleza kuwa TBA wamfuate, badala ya kudai kupitia magazeti.
“He! ndiyo unaniambia wewe, sina taarifa kama wana madai, waje tu siyo kudai kwenye magazeti.” alisema.
Mwingine ni mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ramo Makani (CCM) anayedaiwa zaidi ya Sh2.5 milioni, alipoulizwa na alijitetea kuwa hana taarifa, kwa kuwa alikuwa safarini Masasi Mkoani Mtwara kwenye msiba.
“ Hapa ninapozungumza nawe nipo njiani naelekea Dodoma, sina habari hiyo wewe ndiyo kwanza unaniambia, natoka kuzika,” alisema Makani.
Mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye (CCM), ambaye kwenye orodha hiyo inaonyesha anadaiwa Sh2.4 milioni, alisema kwamba hajawahi kuwa na mkataba na TBA.
“ Eeh! Labda wamekosea sijawahi kuwa na mkataba na TBA mimi,” alijibu Ole Medeye kisha akakata simu.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment