Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, August 31, 2014

CHADEMA YATOA UFAFANUZI JUU YA GHARAMA ZA FOMU NA UMRI WA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI BAVICHA


TAARIFA KWA UMMA
UFAFANUZI JUU YA GHARAMA ZA FOMU, UMRI WA KUGOMBEA, KAMPENI ZA UCHAGUZI NDANI YA BARAZA NA USAILI WA WAGOMBEA
Wakati zoezi la uchukuaji fomu kwa ajili ya kugombea nafasi mbali mbali ndani ya Baraza zikiendelea, tunapenda wanachama hususani vijana kufahamu na kuzingatia mambo yafuatayo:
1. ADA YA FOMU YA KUGOMBEA
Tunapenda kuwajulisha wananchama wote wanaochukua fomu za kuomba nafasi za uongozi wa Baraza kuwa gharama za fomu ni kama ilivyoandikwa kwenye fomu yaani Shilingi 50,000/= kwa nafasi zote. Nafasi hizo ni:
i) Mwenyekiti
ii)Makamu mwenyekiti Bara na Visiwani
iii)Katibu Mkuu wa Vijana
iv)Naibu Katibu Mkuu wa Vijana Bara na Visiwani
v)Mratibu wa uhamasishaji
vi)Mweka Hazina
vii)Wajumbe watano wanaowakilisha Vijana Baraza Kuu
Viii)Wajumbe ishirini wanaowakilisha vijana katika Mkutano Mkuu wa Chama.
2. UMRI WA KUGOMBEA
Kwa mujibu wa kanuni za Baraza, mgombea yoyote anapaswa kumaliza kipindi cha uongozi wake, kama atachaguliwa, akiwa bado na umri wa ujana yaani miaka na kwamba asiwe amezidi miaka 35. Hivyo ni lazima mgombea yoyote asiwe amezidi umri wa miaka 30 wakati anagombea. Kwa maana hii, wagombea wote wa nafasi za uongozi wa BAVICHA Taifa wanapaswa kuwa ni wale waliozaliwa tarehe 10.09.1984 na kuendelea kwani mtu atatambulika kuwa kiongozi wa Baraza Taifa kuanzia tarehe hiyo na si vinginevyo.
Ndio maana tunaendelea kusisitiza kuwa moja ya viambatanisho muhimu vya kwenye fomu ya kugombea kiwe kimojawapo kati ya cheti cha kuzaliwa, hati ya kusafiria au kitambulisho cha kupiga kura na si tofauti na hapo.
3. UREJESHAJI WA FOMU
Hapo awali tulielekeza kuwa siku ya mwisho ya kurejesha fomu ni tarehe 25.08.2014 Saa kumi na nusu jioni na kwamba fomu hizo zirejeshwe makao makuu ya BAVICHA Dar es salaam ama ofisi ndogo za BAVICHA Zanzibar. Tunapenda kuendelea kusisitiza kwamba muda wa mwisho ni kama ilivyopangwa. Hata kama uko mkoani, hakikisha fomu yako inafika makao makuu ya Baraza ndani ya muda uliopngwa.
4 USAILI WA WAGOMBEA
Baraza linapenda kuwafahamisha wale wote wanaokusudia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuwa tarehe 4 na 5 Mwezi Septemba 2014 ndio siku za usahili. Usahili huu utafanyika Jijini Dar es salaam na wagombea wote wanapaswa kufika na vyeti vyao halisi. Gharama za kuwepo Dar es salaam pamoja na usafiri zitakua juu ya wagombea wenyewe.
5 KAMPENI ZA UCHAGUZI NDANI YA BARAZA
Kama ilivyoelezwa hapo awali, Katiba ya chama, Mwongozo wa Baraza, taratibu za uchaguzi za chama toleo la mwaka 2012, na mwongozo wa dhidi ya rushwa wa mwaka 2012, kwapamoja ndio zinaongoza uchaguzi huu.
Pamoja na mambo mengine ya kuzingatia, muda wa kampeni ni wiki moja kabla ya siku ya uchaguzi na si tofauti na hapo. Tunapenda kuwasisitiza vijana wote wa CHADEMA hususani wenye nia ya kugombea kuwa makini katika masuala haya. Tusingependa kuona vijana wanafifisha ndoto zao za kugombea nafasi ndani ya baraza kwa kukiuka tu taratibu hizi.
Imetolewa leo tarehe12.08.2014 Jijini Dar es salaam na;
Ester Daffi
Naibu Katibu Mkuu – BAVICHA
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment