Writen by
sadataley
3:10 PM
-
0
Comments
Wachezaji wa Ujerumani wakiwa katika picha ya pamoja na Kansela Angela
Merkel (katikati), Rais Joachim Gauck (kati kushoto), na kocha wa
Joachim Loew wakishangilia baada ya Ujerumani kutwaa Kombe la Dunia kwa
kuifunga Argentina 1-0 kwenye Uwanja wa Maracana, Rio de Janeiro,
Brazil. Picha na AFP Rio de Janeiro, Brazil. Shujaa wa Ujerumani, Mario Gotze amesema
kufunga bao pekee na la ushindi katika fainali ya Kombe la Dunia ni
kama bahati na zawadi yake katika msimu wake mgumu akiwa Bayern Munich.
Gotze (22), mwenye sura ya kitoto, alituliza
kifuani mpira wa krosi ya Andre Schuerrle kabla ya kupiga shuti kufunga
bao katika dakika ya 113, na kuipa Ujerumani ushindi 1-0 dhidi ya
Argentina kwenye Uwanja wa Maracana, Rio de Janeiro, Brazil.
“Ni hisia ambazo siwezi kuziamini wala kuzielezea,” alisema kiungo huyo wa Bayern.
“Sijui hata nilielezee vipi hili. Unajikuta
unafunga bao na hujui kitu kitakachotokea. Itakuwa ni sherehe pamoja na
timu nzima na taifa kwa ujumla. Ni kama ndoto iliyotimia.”
Gotze aliingia kuchukua nafasi ya mkongwe Miroslav
Klose kabla ya kuanza kwa muda wa nyongeza. Hilo ni bao lake la 11
kuifungia timu ya taifa katika michezo 35 aliyoitumikia miamba hiyo
maarufu kama ‘Die Mannschaft’.
Alitwaa pia tuzo ya mchezaji bora wa mechi, ambayo
alipewa uwanjani hapo wakati Ujerumani ikiweka rekodi ya kuwa timu ya
kwanza kutoka Bara la Ulaya kutwaa taji hilo katika ardhi ya bara la
Amerika Kusini.
Gotze anaungana na ‘Der Bomber’ Gerd Mueller,
ambaye alifunga bao la ushindi kwa Ujerumani Magharibi katika mchezo wa
fainali 1974 mjini Munich, akiwa mchezaji mwingine wa Bayern kulipa
ubingwa taifa hilo.
Gotze alitua nchini Brazil akiwa ametokea kwenye
hali ngumu katika msimu wake wa kwanza na miamba hiyo ya Bavaria, akiwa
ameshindwa kupata nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha kocha
Pep Guardiola.
Akiwa ametwaa mataji mawili ya Bundesliga na
Borussia Dortmund, klabu ambayo alijiunga nayo akiwa na miaka nane,
Gotze alikuwa adui namba moja wa mashabiki wa Borussia Aprili 2013,
alipokubali uhamisho wa Euro 37 milioni ili kujiunga na Bayern.
Uhamisho huo umemfanya nyota huyo kuipa kisogo
timu iliyomkuza na ya nyumbani kwao. Alikuwa nje katika mchezo wa
fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Mei 2013, baada ya kuumia katika
mchezo wa nusu fainali ya michuano hiyo.
No comments
Post a Comment