Writen by
sadataley
4:02 PM
-
0
Comments
Wachezaji wa Colombia wakishangilia baada ya kufunga goli la pili dhidi ya Uruguay na kufuzu kuingia hatua ya robo fainali.
Na Brasilia, BrazilBrasilia, Brazil. Historia mpya imeandikwa Brazil baada ya
washindi wa makundi manane waliofuzu kucheza hatua ya 16 bora kuingia
robo fainali.
Hiyo ni historia mpya tangu kuanza kwa Fainali za
Kombe la Dunia 1930. Orodha hiyo ilikamilishwa juzi baada ya Ubelgiji
kuilaza Marekani 2-1 kwenye muda wa ziada baada ya awali, Argentina
kuiondoa Uswisi, pia kwenye muda wa ziada.
Mafanikio hayo ni mapya tangu kuanza kwa mfumo wa timu 32, hakuna mshangao kwa washindi hao kuingia hatua ya 16 bora.
Safari ya timu zilizofuzu kucheza robo fainali
ambazo ni Brazil, Colombia, Uholanzi, Costa Rica, Ufaransa, Ujerumani,
Argentina na Ubelgiji ilikuwa kama ifuatavyo:
Brazil
Ilimaliza mbele ya Mexico katika Kundi A ikiwa na
pointi saba, ikailaza Chile 3-2 kwa penalti (baada ya sare ya 1-1)
katika hatua ya 16 bora.
Wenyeji Brazil walikuwa na kibarua kuizima Mexico
kwenye makundi vilevile mchezo dhidi ya Chile katika hatua ya 16 bora
ulikuwa mgumu kwao, kiasi kwamba ilikuwa ni bahati kwao, Brazil kufuzu
kwa penalti, pia mabao ambayo alifunga Neymar katika hatua ya makundi
yaliibeba nchi hiyo.
Colombia
Walimaliza mbele ya Ugiriki katika Kundi C wakiwa na pointi tisa na wakailaza Uruguay 2-0 katika hatua ya 16 bora.
Kwa ujumla, Colombia ni timu ambayo imekuwa
kivutio kikubwa katika fainali za mwaka huu. Waliongoza Kundi C
kirahisi, kabla ya kuilaza Uruguay bila mtukutu Luis Suarez. Kibarua
kigumu kwao ni kuwakabili wenyeji Brazil, kesho.
Uholanzi
Walimaliza mbele ya Chile katika Kundi B wakiwa na
pointi tisa, wakaizima Mexico 2-1 katika hatua ya16 bora. Walianza
vyema kwenye hatua ya makundi kwa kuwalaza waliokuwa mabingwa watetezi,
Hispania kwa mabao 5-1 kabla ya kuwaondoa Australia.
Ushindi wao dhidi ya Chile ulikuwa wa kukamilisha ratiba kabla
ya kuivaa Mexico katika mechi iliyokuwa ngumu. Katika mechi hiyo dhidi
ya Mexico, mabao ya ‘jioni’ ya Uholanzi kutoka kwa Wesley Sneijder na
Klaas-Jan Huntelaar yaliwapa tiketi ya kucheza robo fainali katika mechi
iliyochezwa dakika 90.
Costa Rica
Walimaliza mbele ya Uruguay katika Kundi D, wakailaza Ugiriki 5-3 kwa penalti (baada ya sare ya 1-1) katika hatua ya 16 bora.
Ni sahihi kusema timu nyingine saba zilizobaki
zina nafasi ya kutwaa taji hili, lakini Costa Rica wameduwaza wengi.
Wamekuwa wakali mbele ya lango la mpinzani, wakifunga mabao na kuwaziba
midogo wakali kama Italia na England.
Waliwatoa Ugiriki kwa penalti licha ya kucheza wakiwa 10 kwa dakika 60.
Ufaransa
Walimaliza mbele ya Uswisi katika Kundi E wakiwa na pointi saba na wakaiondoa Nigeria kwa mabao 2-0 katika hatua ya 16 bora.
Msimu huu, Ufaransa inamtumia vizuri mshambuliaji wake nyota, Karim Benzema akiwa katikati na wakati mwingine pembeni.
Katika mchezo dhidi ya Nigeria walionekana
kupotea, lakini mabao ya dakika 11 za mwisho ya Paul Pogba na mlinzi
Joseph Yobo aliyejufunga yaliwaokoa.
Ujerumani
Walimaliza mbele ya Marekani katika Kundi G wakiwa na pointi saba na wakaizima Algeria kwa mabao 2-1 kwenye hatua ya 16 bora.
Vita inayowasubiri kwenye Uwanja wa Maracana dhidi
ya Ufaransa ni safari ambayo itatosha kuonyesha kuwa haikuwa ngekewa
kuwatoa Algeria.
Walianza fainali hizi kwa makali kwa kuiadhiri Ureno. Katika
mechi dhidi ya Algeria walionyesha udhaifu kwenye safu ya ulinzi,
wakitegemea miujiza ya Thomas Muller akiwa kwenye kiwango.
Argentina
Walimaliza mbele ya Nigeria katika Kundi F wakiwa na pointi tisa na wakaiondoa Uswisi kwa mabao 1-0 katika hatua ya 16 bora.
Lionel Messi amekuwa ndiye mwokozi wao akiwa na mabao manne kibindoni.
Kwenye makundi walizilaza mapema Bosnia kwa mabao
5-1, Iran na Nigeria, lakini walitegemea miujiza ya Angel Di Maria
kuitupa nje Uswisi katika hatua ya 16 bora.
Ubelgiji
Walimaliza wababe kwa Algeria katika H wakiwa na
pointi tisa na wakaiondoa Marekani kwa mabao 2-1 kwenye muda wa nyongeza
katika hatua ya 16 bora.
Hadi sasa wameshinda mechi zao zote, ingawa sifa
yao imeingia doa kwa kukosa mfumo wa kuaminika wa kushambulia, kiasi cha
kumaliza dakika 52 kwenye mechi zote bila hatari yoyote langoni mwa
wapinzani. Juzi, walibadilika dhidi ya Marekani ambayo mikono ya kipa
Tim Howard imemweka juu kwa kufanikiwa kuokoa michomo 15 ya hatari.
No comments
Post a Comment