Writen by
sadataley
11:04 AM
-
0
Comments
Kama ilivyoada ya jumanne, GK inakupa fursa ya kutazama picha mbalimbali
tulizokusanya kutoka makanisani nchini kujua yaliyojili katika ibada ya
jumapili iliyopita katika makanisa hayo. Kwakuanza tunaanza na mkoani
MWANZA ambako redio ya Kikristo ya HHC iliandaa tamasha la uimbaji
lililofanyika katika viwanja vya kanisa la AIC Nyakato na kuhudhuriwa na
waimbaji pamoja na waumini kutoka madhehebu mbalimbali.
 |
| Waimbaji wakimsifu Mungu. |
 |
| Mmoja kati ya watangazaji wa radio ya HHC Maganga James mwenye shati nyeupe na tai akisikiliza uimbaji. |
 |
| Lemi George akiwaongoza wenzake katika kumsifu Mungu. |
 |
| Hakika ilikuwa safi sana kama inavyoonekana. |
 |
| Mmmh shetani aliipata pata jumapili. |
 |
| Waimbaji wakiwa wametulia wakicheza kwa madaha kumsifu Mungu. © Maganga James Gwensaga. |
Baada ya kutoka Mwanza sasa ni jijini MBEYA ambako GK imefanikiwa kupata
picha hizi za waumini wa kanisa katoliki mitaa ya jiji hilo wakiwa
katika maandamano ya sherehe ya Ekaristi Takatifu ama Mwili na damu ya
Yesu.
 |
| Gari likiwa limebeba bango la sherehe ya ekaristi takatifu. |
 |
| Msafara wa ekaristi takatifu ukisonga mbele. |
 |
| Watawa, waimbaji na waumini katika maandamano hayo. |
 |
| Msafara wa Ekaristi kama unavyoonekana. ©Gershom Willy |
Baada ya mkoani Mbeya na sasa ni huko mkoani KIGOMA ambako GK inapiga
hodi hadi katika kanisa la Ufufuo na Uzima mkoani humo, ambao walikuwa
na ibada nzuri ya matendo makuu ya Mungu kutendeka kama ilivyo kawaida
ya jumapili zote, waumini walisikiliza neno pamoja na kuwa na kipindi
cha kusifu na kuabudu bila kusahau 'Kupiga Majeshi'.
 |
Mikono juu kuonyesha unyenyekevu kwa muumba wao.
|
 |
| Pia ibada hiyo ilikuwa na kipindi kizuri cha uimbaji. |
 |
| Baadhi ya waumini wa kanisa la Ufufuo Kigoma wakiwa ibadani. |
 |
| Jopo la watumishi wa kanisa la Ufufuo na Uzima Kigoma. ©Ufufuo Crew. |
Baada ya mkoani Kigoma na sasa tunaelekea jijini Arusha ambako jumapili
wapenzi wa muziki wa injili waliofika katika ukumbi wa hoteli ya
Corridor Springs ya jijini humo walipata wasaa mzuri wa kushuhudia live
recording iliyohusisha kwaya ya Tumaini Shangilieni pamoja na kwaya
marafiki kutoka Mombasa Kenya ambao kwa pamoja kupitia sare zao nadhifu
zenye kuonyesha bendera za nchi yao, walionekana wenye kupendeza na
nadhifu haswa. Bila kusahau mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Beatrice
Muhone alikuwa sambamba kumtukuza Mungu na kwaya yake iliyomlea ya
Tumaini.
 |
| Mambo yalikuwa mazuri kwakweli kama wanavyoonekana. |
 |
| Wapigaji wa muziki wa kwaya ya Tumaini shangilieni wakiwajibika. |
 |
| Tumaini na wageni wao wakiwa jukwaani. |
 |
| Kwaya ya Upendo St. James wakimsifu Mungu. |
 |
| Baadhi ya waimbaji wa Tumaini, mbele na kwaya ya Mombasa nyuma yao wakiwa wametulia katika ukumbi huo. |
 |
| Angel akiwa na mwimbaji mwenzake wa Tumaini Beatrice Muhone wakiwa katika pozi la picha. |
 |
| Baadhi ya wadada wa Shangilieni wakiwa katika pozi. ©Angel Minja & Samuel Kusamba. |
Baada ya jijini Arusha sasa ni mkoani DAR ES SALAAM ambako tunaanzia
huko mitaa ya Goba Matosa, katika kanisa la Tanzania Assemblies of God
(T.A.G) City Light Temple kwa mchungaji Nimrodi Swai ambao licha ya
ibada ya jumapili, walikuwa pia na mkutano wa Kiroho ambao ulifanyika
baraka kwaa watu waliohudhuria.
 |
| Waumini wakiwa wamekaa kwa utulivu kusikiliza mkutano huo. |
 |
| Kila mmoja alisimama au kukaa palipomfaa ili kusikiliza kilichokuwa kikiendelea. |
 |
| Mtumishi wa Mungu akipaza sauti ya ukombozi. |
 |
| Ilikuwa shangwe sana katika kumsifu Mungu. ©Sam Steven |
Baada ya kutoka Goba, GK ikajisogeza mjini katika usharika wa Kilutheri
Kijitonyama ambako kulikuwa na ibada kama kawaida, ambapo jumapili
iliyopita walipata wageni Ukombozi kwaya kutoka Lutherani Msasani jijini
Dar es salaam, ambao walifanyika baraka usharikani hapo kwa uimbaji
wao.
 |
| Mrs Margaret Kato akiwaimbisha waimbaji wenzake wa Ukombozi Msasani. |
 |
| Ukombozi Kwaya wakimsifu Mungu. |
 |
| Kijitonyama Uinjilisti wakishambulia jukwaa. |
 |
| Modest Morgan akiliongoza kundi la Kijitonyama Uinjilisti kumsifu Mungu. ©Onai Joseph |
No comments
Post a Comment