Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, June 16, 2014

UMOJA WA KINA BABA WAZINDULIWA, NA KUONGOZA IBADA YA KUPENDEZA K.K.K.T MWENGE

Jumapili iliyopita ya tarehe 8 mwezi huu wa sita ilikuwa ni jumapili ya tofauti katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (K.K.K.T) Usharika wa Mwenge jijini Dar es salaam, ambapo Usharika huo ulipata kwa mara ya kwanza umoja wa wanaume kanisani hapo (wakinababa) ambapo pia walishika hatamu ya kuongoza ibada.
Yafuatayo ni baadhi ya matukio katika picha jinsi hali ilivyokuwa katika Ibada hiyo iliyoongozwa na Wanaume
SIFA ILICHUKUA NAFASI
Mwalimu Kahesi akiongoza nyimbo za kuabudu na kusifu
Baadhi ya waumini waliohudhuria.
Ilikuwa furaha uweponi mwa Bwana

Kila mmoja akimtafakari Mungu usharikani hapo.

KWAYA YA WANAUME
Ilipendeza sana, sauti zote zilitoka kwao.

Kupendeza nayo wee.





NENO LILICHUKUA NAFASI YAKE
Mchungaji wa Usharika wa Mwenge mchungaji Kanisa Msangi akiongoza maombi .Pembeni yake ni mzee Godlisten Lema aliyeongoza Liturjia



Mwinjilisti akihubiri kwenye ibada ya wanaume jumapili.

Mzee wa kanisa Godlisten Lema akiongoza Ibada jumapili.


IGIZO NALO LILIKUWEPO

Vijana wakiigiza igizo katika ibada hiyo






UONGOZI
 
Viongozi waliochaguliwa kuongoza Umoja wa wanaume wakiwa kwenye picha ya pamoja
Kutoka Kushoto ni bwana Johanes Makundi,(mweka hazina msaidizi, bwana Nathaniel Minja (mweka hazina), Mzee Tumaini Kichila  mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya ibada ya wanaume na mwenyekiti wa kamati ya mahusiano ,bwana Allen Mushi (katibu msaidizi), bwana Denis Ndyetabula (katibu), bwana Leonard Mushi (makamu mwenyekiti) na bwana Jonas Mbise (mwenyekiti) wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uchaguzi wa viongozi hao
BAADA YA IBADA
Baadhi ya wanaume wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya ibada.©Tumaini Kichila



Picha zote kwa hisani ya Tumaini Kichila
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment