Writen by
sadataley
5:23 PM
-
0
Comments
Mkutano mkuu wa taifa wa 49 wa umoja wa wanafunzi wa Kikristo Tanzania
(UKWATA) umemalizika siku ya jana katika chuo cha ualimu Korogwe
ikishuhudiwa umoja huo ukipata viongozi wapya pamoja na mkoa wa Iringa
kuibuka mabingwa kwenye mashindano ya uimbaji.
Viongozi waliochaguliwa kushika hatamu ya mwaka 2014/2015 ni pamoja na
Rais wa umoja huo bwana Laban Ndomkwa, makamu wake akiwa Vestina Sai,
Katibu ni kijana Edward Kasawala, msaidizi wake ni mwanadada Neliwa
Samweli huku mtunza fedha wa umoja huo akiwa Gerson Living. Pamoja na
mengi yaliyotendeka ikiwa pamoja na vipindi vya maombi pamoja na neno
ambavyo vimeshuhudia wanafunzi mbalimbali kufunguliwa na kusimamishwa
upya ikiwa ni moja ya lengo la mkutano huo.
Aidha pia katika suala la uimbaji mkoa wa Iringa umeibuka mabingwa kama
ilivyotabiriwa kutokana na uimbaji wao wakichukua jumla ya maksi 156.5
za majaji wakifuatiwa na mkoa wa Dar es salaam na Pwani ambao huitwa
DARPWANI waliochukua jumla ya maksi 156, namba tatu ilichukuliwa na
wenyeji mkoa wa Tanga kwa jumla ya maksi 151 huku Ukwata kutoka makao
makuu ya nchi mjini Dodoma wakiondoka na nafasi ya nne kwa maksi 145.5
 |
| Rais mpya wa Ukwata Tanzania Laban Ndomkwa. |
 |
| Makamu wa Rais Ukwata Tanzania Vestina Sai |
 |
| Katibu mkuu Ukwata Tanzania Edward Kasawala |
 |
| Katibu msaidizi Neliwa Samweli |
 |
| Mtunza fwedha Ukwata Tanzania Gerson Living. |
 |
| Mambo ya uchaguzi yalivyokwenda. |
 |
| Orodha ya viongozi wapya Ukwata Tanzania. |
 |
| Wanaukwata wakipanda mabasi tayari kurejea makwao asubuhi ya leo. |
 |
| Wakati kama huu huwa mbaya sana kwa wanafunzi wengi hasa baada ya kutengeneza marafiki kutoka kila kona ya nchi. |
 |
| Safari salama mko na Yesu. shukrani kwa mwana GK na mdau wetu mkubwa Onai Joseph kwa matukio yote haya. |
No comments
Post a Comment