Writen by
sadataley
10:33 AM
-
0
Comments
Dar na Dodoma. Sakata la nani mmiliki halali wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda), limeendelea kuchukua sura mpya. Wakati Mbunge wa Temeke (CCM), Abbas Mtemvu akitoa tuhuma kwamba limeuzwa kinyemela, Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Simon Group, Robert Kisena ameibuka na kudai kuwa halikuwahi kuuzwa.
Juzi, akichangia mjadala wa Bajeti wa Wizara ya
Fedha, Mtemvu alisema kulifanyika ujanjaujanja kati ya Simon Group na
Meya wa Jiji, Didas Masaburi kukopa benki na taasisi nyingine kwa ajili
ya kununua kampuni hiyo.
Mtemvu alisema baada ya Simon Group kuuziwa Uda
kwa bei poa, wahusika walishindwa kulipa fedha hizo ndipo (wadai)
walipokwenda mahakamani na kutaka walipwe chao.
Alisema baada ya kampuni na benki walizokopa
kushinda kesi mahakamani, kampuni moja ya udalali ilipewa kazi ya
kuipiga mnada depo ya Uda na Februari 23, ilinunuliwa na Jazeera kwa
Sh12bilioni.
Jana, Mtemvu alisema: “Tunaambiwa kulikuwa na
zuio, hapa tunataka kujua, kwanza huyu aliyeweka hati za Uda kwa zuio
isipigwe mnada... utaratibu uliotumika kuiuza Uda, hapa kuna mchezo
mchafu umefanyika, iweje mambo yafanyike bila wadau, wahusika wa mkoa
kushirikishwa?”
Alisema Uda haiwezi kuuzwa kwa bei chee ya Sh280
milioni... “Ina viwanja Stesheni, ina nyumba Msasani, Chang’ombe, Ilala
Sharif Shamba, Kijitonyama, Upanga hivi vyote ni zaidi ya Sh280
milioni.”
Katika maelezo yake bungeni juzi, Mtemvu alisema
wabunge wa Dar es Salaam hawakatai kubinafsishwa kwa Uda ila wanataka
uhalali na haki katika ubinafsishaji huo.
Kisena
Akizungumza jana, Kisena alisema Uda haijauzwa na
hawana mpango wa kuiuza na akahusisha tuhuma hizo na mkakati mbaya
unaofanywa na baadhi ya watu wasiopenda maendeleo ya shirika hilo.
“Mimi ndiyo kwanza nasikia habari hizo eti Uda imeuzwa kwa Kampuni ya Jazeera… sijui kwa nani… huo ni uzushi.
Nenda kwa Mtemvu akupe document (nyaraka) za
uuzwaji wa Uda… akwambie iliuzwa lini na kwa sababu zipi na kama iliuzwa
kwa madeni ni benki gani inadai ili uweze kufuatilia na kuuambia umma
ukweli.”
“Watu wote watambue kuwa Uda inamilikiwa na watu
wawili: Simon Group na Serikali kupitia Msajili wa Hazina na hakuna
mmiliki mwingine na halijauzwa. Hii kampuni ni kubwa sana hivi iuzwe
bila waandishi wa habari na umma kujua na mnada hutangazwa siku 14
kabla… yaani siku zote zipite watu wasijue?” alihoji Kisena.
Kwa habari zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Sura-mpya-ya-sakata-la-Uda/-/1597296/2338850/-/1qf3irz/-/index.html
Kwa habari zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Sura-mpya-ya-sakata-la-Uda/-/1597296/2338850/-/1qf3irz/-/index.html
No comments
Post a Comment