Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, June 25, 2014

Raia wa Libya kuwachagua wabunge wapya


Uchaguzi nchini Libya
Upigaji kura umeanza nchini Libya ambapo raia wanachagua bunge jipya.
Bunge hilo litachukua nafasi ya baraza la kitaifa ambalo limekuwa likikumbwa na migawanyiko ya kisiasa na kimawazo kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Huu ni uchaguzi wa pili kufanyika nchini humo tangu kumalizika kwa mapigano yaliyomng'oa mamlakani aliyekuwa kiongozi wa mda mrefu Muamar Ghaddafi .
Wananchi wa Libya wanaendelea kupiga kura kuchagua wabunge wapya.
Wanatumaini kuwa huu utakua mwanzo mpya baada ya malumbano ya kisiasa yaliyoshuhudiwa tangu kuchaguliwa kwa bunge la kwanza mwaka 2012.
Inaelekea kuwa idadi ya wapigaji kura ni ndogo ikilinganishwa na idadi ya wapigaji kura waliosajiliwa.
Wagombea wapatao 2000 wanagombea nafasi 200 za ubunge.
Kutokana na hofu ya usalama idadi ya waangalizi wa kimataifa ni chache.
Eneo la mashariki la Libya limekuwa likikabiliwa na machafuko yanayoshukiwa kuchochewa na makundi ya wanamgambo.
Maafisa wa uchaguzi wanatarajia shuguli za upigaji kura kutatizwa katika baadhi ya miji.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment