Writen by
sadataley
5:11 PM
-
0
Comments

mashabiki wa Costa Rika wakisherehekea
Makumi ya maelfu wa raia wa Costa Rica wamesherehekea
ushindi wa timu yao ya taifa katika mechi za kombe la dunia
zinazoendelea nchini Brazil baada ya kuishinda italy kwa bao moja kwa
bila.
Raia hao waliokuwa wakipeperusha bendera
walisherehekea ushindi huo ambao umewaweka katika nafasi nzuri ya
kuingia katika awamu ya mchujo kwa mara piliUshindi huo pia unamaanisha kuwa Uingereza imebanduliwa nje ya mashindano hayo .
Wakati huohuo Ufaransa imepanda hadi katika nafasi ya kwanza ya kundi E baada ya kuicharaza Switzerland kwa mabao matano kwa mawili.
Katika mechi za kundi jengine Ecuador iliishinda Honduras kwa mabao mawili kwa moja katika mechi iliojaa msisimuko mkubwa.
No comments
Post a Comment