Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, June 16, 2014

Operesheni ya utumbo wa mtoto pacha yafanikiwa


Daktari wa watoto mapacha waliokuwa wameungana akiwa amewabeba mara baada ya kufanywa upasuaji hivi karibuni. Picha na Maktaba 
Na Peter Elias, MwananchiDar es Salaam. Hatimaye mtoto Eliud, mmoja kati ya pacha waliokuwa wameungana kabla ya kutenganishwa kwa upasuaji huko India Februari, mwaka huu, ameanza kwenda haja kubwa kwa njia ya kawaida baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo na kurudishwa ndani sehemu ya utumbo iliyokuwa imetoka nje.
Upasuaji huo ulifanywa Ijumaa iliyopita katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na jopo la madaktari bingwa kutoka Misri.Baada ya kurejea kutoka India na kisha kwenda Mbeya, Eliud alipata tatizo la utumbo mkubwa kutoka nje na kutopenda kula, hali iliyomfanya adhoofu.
Jana, baba mzazi wa pacha hao, Eric Mwakyusa alisema upasuaji huo ulifanikiwa na sasa mtoto huyo anaendelea vizuri... “Ninamshukuru Mungu sasa Eliudi anakula na kwenda haja kubwa kwa njia ya kawaida. Kwa sasa tunauguza kidonda tu.”
Daktari anayewasimamia watoto hao, Zaituni Bokhary hakupatikana kuzungumzia hali za pacha hao lakini Mwakyusa alisema madaktari hao wako karibu na pacha hao kujua maendeleo yao.
Mwakyusa alisema pacha mwingine, Elikana ambaye pia alikuwa na tatizo la utumbo kutoka nje kwa kiasi kidogo ikilinganishwa na Eliud, atafanyiwa upasuaji... “Kurudisha utumbo ndani na kuziba tundu.”
Watoto hao wanatarajiwa kurejea India Agosti, mwaka huu kwa ajili ya upasuaji mwingine.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment