Writen by
sadataley
11:33 AM
-
0
Comments

Wasichana
waliyotekwa nyara na kundi la Boko
Raisi wa zamani wa Nigeria Olesegun Obasanjo ameonyesha hofu yake kuwa huenda wasichana waliotekwa na boko haram hawatapatikana
wote wakati huu tukio la kutekwa kwa wasichana hao limetimiza miezi
miwili hii leo tangu kutokea huku bado juhudi za kuwatafuta zikifanywa
na wataalamu mbalimbali wa kimataifa wakilisaidia jeshi la Nigeria.
Akihojiwa na mtandao mmoja wa habari huko Nigeria bwana
Obasanjo amesema kuwa hashawishiki kuamini kuwa wasichana hao wataweza
kupatikana wote vinginevyo itakuwa miujiza.
Wapiganaji wa Boko Haram waliwateka wasichana wa shule takribani 276 katika shule moja katik akijiji cha Chibok, katika jimbo la kaskazini mashariki la Borno mnamo tarehe 14 mwezi wa nne.
Ni miezi miwili sasa, kuna dalili kidogo za wasichana Kuachiwa huru au kuokolewa, licha ya jeshi la Nigeria kusema kwamba walijua wapi wasichana walipofichwa baada ya kutekwa na jitihada za kimataifa kuendelea.

No comments
Post a Comment