Writen by
sadataley
11:00 AM
-
0
Comments
![]() |
| Mchungaji Jeremy Pemberton kushoto akiwa na rafikiye wa kiume baada ya kuoana kitendo ambacho ni marufuku kwa wachungaji wa kanisa hilo kukitenda. |
Kanisa la Anglikana nchini Uingereza limemzuia mchungaji wake wa kwanza kuoana na mwanaume mwenzake toka kanisa hilo lilipopitisha ruhusa ya ndoa za jinsia moja mapema mwaka huu, kutoendelea kuongoza ibada na badala yake ametakiwa kusimamia utumishi katika hospitali ya Lincoln.
Canon Jeremy Pemberton ambaye alipata pongezi kutoka chama cha watetea haki wa ndoa za jinsia moja cha LGBT alipofunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi, haruhusiwi kuongoza ibada huko Nottinghamshire na badala yake ataendelea na kazi yake ya kuwa mchungaji katika hospitali ya Lincoln. Mchungaji Pemberton ambaye ni alikuwa mmishenari wakati huo, amekataa kuzungumza lolote na wanahabari kuhusiana na hatua hiyo.
Kwa mujibu wa kaimu askofu wa Dayosisi jimbo la Southwell na Nottingham nchini Uingereza mchungaji Richard Inwood akizungumzia hatua hiyo amesema mafundisho ya kanisa hilo yanakwenda sambamba na maisha halisi ya watumishi wa kanisa hilo na kuongeza kwamba alishazungumza na mchungaji Pemberton juu ya uamuzi huo nakumwambia majukumu yake katika jimbo hilo yamebadilika.
Onyo hilo limekuja wakati jumamosi iliyopita mchungaji mwingine wa kanisa hilo Andrew Cain wa kanisa la Mtakatifu James lililopo West Hampstead jijini London kufunga ndoa na mwanaume mwenzake ambaye wamekuwa na mahusiano naye kwa muda mrefu, kwa upande wake alipokea kwa masikitiko uamuzi uliotolewa juu ya mchungaji mwenzake na kuamua kuandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Twitter kwamba hatua hiyo ni aibu, ni uamuzi mbaya na kwamba kanisa hilo linapopiga hatua na wenyewe wanapiga hatua mbele, akamalizia kwakusema uamuzi huo ni upumbavu na wa makosa.
![]() |
| Mchungaji Andrew Cain kulia akiwa mwenye furaha baada ya kufunga ndoa jumamosi iliyopita na rafikiye. |
Hatua ya kanisa Anglikana Uingereza kuweka sheria kwa wachungaji wake kutooana na watu wa jinsia moja inadaiwa ni shinikizo la maaskofu kutoka bara la Afrika ambao wanawakilisha waumini takribani milioni 35 barani humu la kutaka vitendo hivyo kupigwa marufuku ama Afrika ijiondoe kwenye ushirikiano na kanisa hilo mama la nchini Uingereza, jambo ambalo askofu mkuu wa kanisa Anglikana Justin Welby hataki kuona Afrika inajitegemea kama kanisa.


No comments
Post a Comment