Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, June 3, 2014

MATUKIO YA WIKI KUTOKA MAKANISANI TANZANIA.

Angalia baadhi ya picha kuwakilisha matukio yaliyojili makanisa mbalimbali nchini Tanzania mwishoni mwa wiki iliyopita.


KIGOMA

Kutoka mkoani Kigoma kanisa la FPCT Kilimahewa kulifanyika mkutano wa injili ambao ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kanisa la FPCT mkoani Kigoma na katika mkutano huo ambao muhubiri alikuwa mchungaji Amos T. Hulilo na mfundishaji wa semina za ndani alikuwa Dkt. Moses Wangira. Katika mkutano uo kuna watu walimpa Kristo maisha yao.


Baadhi ya wachungaji na watumishi wa kanisa la FPCT Mkoani Kigoma wakiwa katika mkutano huo.
Maombi yalifanyika kwa watu wenye shida mbalimbali kama inavyoonekana©FPCT Kigoma

ZANZIBAR
Katika kanisa la Assemblies of God (T.A.G) Zanzibar City Christian Centre la Kariakoo visiwani Zanzibar kulifanyika sikukuu ya watoto ambayo ilipendezwa na watoto ambao walisimama katika zamu zao wakiongozwa na baba wa usharika Askofu Kaganda.

Watoto wakimsifu Mungu katika ibada hiyo.

Askofu Kaganda akizungumza katika ibada hiyo.
Baadhi ya umati wa waumini pamoja na watoto katika ibada hiyo ©Zanzibar Christian Centre

DODOMA

Kutoka makao makuu ya nchi mkoani Dodoma GK imebahatika kupata picha hizi za ibada takatifu ya matendo makuu ya Mungu kutoka katika kanisa la TAG Calvary Christian Assembly.

Neno lilihubiriwa.
Waimbaji walirudisha sifa kwa Mungu.
Uweponi Mwake watu walijisogeza © Willy Mongi

ARUSHA

Katika usharika wa St. James Anglikana Arusha, mwimbaji nyota wa kwaya ya Tumaini Shangilieni aitwaye Mathayo Lemabi alizindua kanda yake ya kwanza akisindikizwa na kundi la Upako la usharikani hapo pamoja na vikundi vingine, huku kwaya ya Tumaini nayo inatarajiwa kuzindua DVD yake ya 5 iitwayo Nisamehe siku ya tarehe 8 yaani jumapili ijayo kanisani kwao.


Mathayo akimsifu Mungu.
Upako wakimsindikiza vyema Mathayo. 
Kazi njema ilifanyika usharikani hapo © Angel Minja

SINGIDA

Kwaya maarufu nchini ya wana ng'ang'ania baraka za BWANA ama waite AIC Shinyanga kwaya walikuwa mkoani Singida kwa mwaliko wa kihuduma ambao uwepo wa Mungu ulikuwa pamoja nao.
Baadhi ya waimbaji wa AIC Shinyanga wakimsifu Mungu.

 DAR ES SALAAM

Ndani ya jiji la Dar es salaam, GK imebahatika kupata picha za tukio la ibada ya jumapili kutoka kanisa la Moravian Uhuru ambao ndiko makao makuu ya kwaya iliyojizolea umaarufu miaka ya karibuni Efatha kupitia wimbo wao 'Twaomba Amani' kwasasa wanapatikana maeneo ya Msimbazi mseto jijini Dar es salaam kutokana na kanisa lao la Kariakoo kutotosha waumini wote hivyo ibada kuamishiwa katika kiwanja cha kanisa hilo mitaa ya Msimbazi ambako kanisa hilo wanapaita Kaanani, katika kanisa hilo jumapili iliyopita kulifanyika siku kuu ya Vijana na kuialika kwaya kongwe jijini humo ya AIC Dar es salaam kutoka Magomeni ambao walimtukuza Mungu pamoja na kwaya wenyeji na kupendezesha sikukuu hiyo ya Vijana.

Baadhi ya waimbaji wa AIC Dar es salaam kwaya stejini wakimsifu Mungu.
Wana wa Aturuzukuye wakiimba sifa kwa Mungu.
Kwaya ya kati ya Uhuru Moravian waite Winners wakimsifu Mungu katika ibada hiyo © Nsajigwa Tufingene.

Pamoja na hayo pia kulikuwa na tendo muhimu sana ndani ya jiji hilo, kwani blogger maarufu wa blog ya Unclejimmytemu bwana James Temu  alikuwa akimvalisha pete ya uchumba mpenzi wake wa karibu mwanadada Sia Kimaro, ubwabwa kuliwa hivi karibuni. GK inawaombea safari njema kuelekea ndoa hadi maisha ya furaha na baraka maisha yao yote.
Pete hiyo si unaona mwenyewe, nimesema mimi ukafikiri labda nadanganya haya sasa.

Nilikwambia mimi, James alipiga goti ooh ukafikiri nakudanganya, ona mwenyewe mpaka raha
Walikuwepo wote mpaka bwana harusi mpya mpya pembeni mwenye shati la drafti bwana Prosper Mwakitalima. 
Kijana mwepesiiii, kashamvisha pete mtu basi aah full tabasamu.
Ndio nshakuvisha hiyo ulifikiri nadanganya…? hihihi GK inadhani labda ndio maongezi yalikuwa yakiendelea.© Samuel Sasali.

Kwa upande mwingine ni tukio la Mchungaji Peter Mitimingi na mkewe Subilaga walifika madhabahuni kumbariki mtoto wao waliyempata hivi karibuni aitwaye Pleasure Mitimingi. Angalia picha chini.



Picha yetu ya mwisho kwa leo ni kutoka mitaa ya Kigamboni katika huduma ya  Mlima wa mabadiliko inayoongozwa na mtume Mary Lutumba sambamba na na mumewe ambaye pia ni mwimbaji maarufu Papaa Lutumba, ibada ilikuwa ya baraka na matendo makuu ya Mungu.

       hABARI KWA HISANI YA http://www.gospelkitaa.co.tz/
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment