Writen by
sadataley
10:52 AM
-
0
Comments

Ni kilio nchini Kenya wakulima wakohofia kupoteza ajira
Marufuku ya utafunaji wa miraa
nchni Uingereza inaanza kutekelezwa leo, nchini Uingereza. Mmea huo
hutafunwa na watu wengi wenye asili ya kisomali , Yemen na Ethiopia,
Serikali ya Uingereza inasema kuwa kuharamishwa
kwa Miraa nchini Uingereza inaambatana na hatua zilizochukuliwa na
mataifa mengine ya Ulaya pamoja na Marekani ambako Miraa ni haramu.Watumiaji wa mmea huo wanasisitiza kuwa sio hatari kuutumia na kwamba kuupiga marufuku ni ubaguzi dhidi ya jamii ambazo ni za wachache.
Mmoja wa watu ambao wamekuwa wakiutumia mmea huo, Aden Haj anasema alitelekezwa na familia yake ambayo haingeweza kustahamili utumiaji wake wa Miraa na anawataka watu kufahamu athari za kutumia Miraa.

Majani ya Miraa ambayo Uingereza inasema ni sawa na dawa za kulevya
Hatua hiyo inajiri baada ya Uingereza kuharamisha utafunaji wa miraa nchini humo baada ya mmea huo kuorodheshwa miongoni mwa madawa ya kulevya.
Uingereza ni mojawepo wa mataifa ya bara Ulaya yaliyokuwa yakitoa soko kubwa zaidi kwa zao la miraa kutoka Kenya kutokana na idadi kubwa ya watu wa jamii ya wasomali wanaoishi nchini humo.
No comments
Post a Comment