Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, June 17, 2014

Kesi za watoto kupewa kipaumbele


Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman.PICHA|MAKTABA 
Na James Magai, MwananchiDar es Salaam. Mahakama imefanya mabadiliko katika kanuni za uendeshaji wa mashauri ya watoto, kwa kuandaa kanuni mpya kwa lengo la kuharakisha usikilizwaji na uamuzi wa kesi zinazowahusu.
Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman alisema hayo wakati wa ufunguzi wa warsha ya uendeshaji wa mashauri yenye masilahi kwa umma, kwa majaji wa Mahakama Kuu, iliyofanyika Dar es Salaam jana.
Jaji Othman alisema mbali na kesi hizo zenye masilahi kwa umma, kesi nyingine ambazo Mahakama inazipa kipaumbele katika kuhakikisha kuwa zinashughulikiwa haraka ni kesi za jinsia na watoto. “Kwa sasa tumeandaa na kuchapisha kanuni mpya za uendeshaji wa mashauri ya watoto. Jambo jipya ni kwamba tunataka usikilizwaji wa kesi za watoto usichukue zaidi ya siku moja na anaweza kuwakilishwa na mtu mwingine,” alisema Jaji Othman.
Alisema hatua hiyo imetokana na utafiti uliofanyika katika nchi tatu za Afrika Mashariki kuhusu uendeshaji wa mashauri yenye masilahi kwa umma ambao umeonyesha kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Kuungana katika Utawala (IGA), Profesa Peter Maina alisema kuna haja ya kutafsiri sheria zote nchini kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili, pamoja na kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa kesi katika ngazi zote za Mahakama kuruhusu kutumia Kiswahili.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment