Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, June 24, 2014

Kesi ya Liz yaanza kusikilizwa Kenya


Liz alibakwa mwaka jana na kuachwa na majeraha mabaya mwilini mwake
Kesi dhidi ya mshukiwa mmoja wa ubakaji aliyekuwa miongoni mwa genge la watu waliombaka msichana mmoja kwa Jina Liz mwaka jana ,na kumtupa ndani ya shimo, inaanza kusikilizwa leo.
Mshukiwa huyo alikuwa mmoja wa watuhumiwa ambao polisi waliwapa adhabu ya kukata nyasi kwa kitendo cha ubakaji na kisha kuachiliwa.
Kesi ya Liz ilisababisha ghadhabu sana sio Kenya tu bali duniani kote hasa kwa ambavyo polisi waliishughulikia.
Mnamo Jumatatu mamia ya wanawake waliandamana mjini Busia ambako kesi hiyo inafanyika wakiunga mkono haki kwa Liz huku kesi hiyo ikianza kusikilizwa.
Muungano wa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayopinga dhuluma dhidi ya wanawake, uliongoza waandamanaji ambao baadaye walikusanyika katika kituo cha mkuu wa jimbo, Isaiah Nakoru.
Walimkabidhi mkuu huyo nyaraka zilizotiwa saini kutaka Liz atendewe haki.
Wanaharakati waliandamana wakitaka Liz kutendewa haki
Waliotia saini nyaraka hizo wanamtaka mkuu wa polisi kuwakamata washukiwa na kitendo hicho cha unyama dhidi ya Liz ambao walimbaka na kisha kutupa mwili wake ndani ya shimo lenye urefu wa futi 25 mjini humo.
Viongozi wa maandamano wanasema kuwa idadi kubwa ya wasichana waliobakwa tangu kusikika kwa kisa cha Liz wamekuwa wakienda kuwashitaki watuhumiwa kwa polisi.
Liz alibakwa na wanaume sita ambao walimuwacha na majeraha mabaya kwenye mwili wake kiasi cha kulazwa hospitalini kwa miezi kadhaa.
Mamake Liz alikuwa miongoni mwa waandamanaji.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment