Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, June 1, 2014

Hili Treni lenye Rangi Mbili UKAWA Hawakuliona wakapanda tu?

Kwa muda mrefu watu walikuwa wanasubiri treni liwapeleke kule walikokuwa wanatarajia kwenda kwa muda mrefu. Walisubiri na kusubiri na hatimaye siku ya siku treni likaja. Halikuwa lile walilolisubiria lakini kwa vile walikuwa wanataka watoke hapo stesheni waliposubiri kwa muda mrefu wakaamua kupanda tu; na mizigo yao na magodogodo yao mengine. Treni liliandikwa mbele "Dodoma"; lilikuwa limeandikwa kwenye kila behewa lake

Kwa muda mrefu watu walikuwa wanasubiri treni liwapeleke kule walikokuwa wanatarajia kwenda kwa muda mrefu. Walisubiri na kusubiri na hatimaye siku ya siku treni likaja. Halikuwa lile walilolisubiria lakini kwa vile walikuwa wanataka watoke hapo stesheni waliposubiri kwa muda mrefu wakaamua kupanda tu; na mizigo yao na magodogodo yao mengine.
Treni liliandikwa mbele “Dodoma”; lilikuwa limeandikwa kwenye kila behewa lake CCM. Treni hili lilipakwa rangi ya njano na kijani na kulifanya lipendeze; na tena lilionekana kama treni jipya kabisa. Ndani kwenye makochi tena madaraja yote – daraja la kwanza hadi daraja la tatu (lenye kubeba watu 201) kila sehemu kulikuwa na alama za jembe na nyundo zikikumbatiana kama wapenzi wasiota kuachana.
Treni lilitangazwa kuwa linakuja na si mwingine bali mmiliki wa treni hilo ambaye naye alifanya hivyo akiwa amevaa mavazi yake yote mawili – la kazi na lile la kitreni! Na treni liliposimama stesheni kuchukua abiria wetu tuliona kuwa tayari lilikuwa limejaa abiria wengine wengi tena karibu asilimia themanini wakiwa wamevaa magwanda yao ya kijani na njano, wakipunga bendera zao za chama wakiimba kwa furaha – CCM Nambari Wani, Twende Dodoma! Na hata kwenye lile libichwa likubwa la treni dereva alikuwa ni MwanaCCM mkongwe kabisa akisaidiwa na Mwana CCM mwingine!
Wasafiri wetu waliona haya yote, walijua haya yote, na walikubali kupanda treni hili. Wenyewe wanasema “waliamini mwenye treni ana nia njema”! Kwamba pamoja na treni kupakwa rangi ya CCM, kuwa na nembo na alama za chama, kuwa na makondakta wa chama na dereva wa chama bado waliamini kuwa mwenye treni alikuwa na nia njema!
Sasa cha kushangaza ni kuwa treni kweli likaondoka stesheni kuelekea Dodoma! Na safari ikiwa imeanza na kunoga wana CCM kwenye treni wanaanza kushangilia; wanaagiza misosi ya KiCCM, radio zinatangaza wanayotaka wao, na wameshikilia nafasi zote wao (chache wamewaachia baadhi ya abiria wetu kuwaonesha ‘nia njema’). Abiria wetu waliokuwa wana hamu sana na hii safari sasa wameanza kucharuka; wanaona mbona treni linaenda kiCCM; mbona mabehewa hadi mlio wa honi umekaa ki CCM? Wanajiuliza. Wengine wanatishia kuteremka kabla ya mwisho wa safari!
Mimi najiuliza, hili treni lilipokuwa linakuja hadi wanaingia ndani walikuwa wamezibwa macho!?
kwa habari zaidi ingiaHili Treni lenye Rangi Mbili UKAWA Hawakuliona wakapanda tu?
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment