Writen by
sadataley
11:51 AM
-
0
Comments
Akizungumza kupitia Redio Maria, wakati wa
kongamano la nne la kitaifa la Utoto Mtakatifu wa Yesu iliyofanyika
katika Kanisa la Mt. Francisco Xvael, wilayani Tunduru Masasi jana, rais
wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Tarcisius Ngalalekumtwa
alisema mauaji ya watoto hivi sasa yanatisha.
Kongamano hilo ambalo lilifanyika ikiwa sehemu ya
madhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, Askofu Ngalalekumtwa alisema
mauaji ya watoto kwa sasa yanapangwa na baba na mama.
“Wakati mwingine baba na mama wanaamua kuwa huyu
mtoto hatumtaki, wanaamua kumnyonga, ni mauaji yanayotekelezwa na
wazazi,” alisema maombi na sala zinahitajika kuikabili hali hiyo.
Hata hivyo, alionya kuwa mauaji hayo hayastahili
kufanywa na jamii kwani kunyonga watoto ni kuondoa uhai wa Mwenyezi
Mungu ambaye alimuumba kwa mfano wake.
Alisema ujumbe wa mwaka huu katika siku hiyo ni
Kupata Elimu Bora Bila Vikwazo ni Haki ya Mtoto na kusisitiza kila mzazi
anapaswa kutekeleza kwa vitendo.
Askofu Ngalalekumtwa alisema jamii ina jukumu la
kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora. Alitoa wito kwa viongozi wa
kisiasa kudumisha amani nchini, Afrika na ulimwenguni.
Kuelekea maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika,
kituo cha luninga cha TV 1 kimezindua shindano kwa vituo vinavyolea
watoto na mshindi ataibuka na kitita cha Sh3.2 milioni.
Taarifa iliyotolewa jana, ilisema shindano hilo
litaendeshwa kwa pamoja na wahisani wa Reach the Change ya Sweden, na
litajulikana kwa jina la Game Changers.
No comments
Post a Comment