Writen by
sadataley
2:18 PM
-
0
Comments
Kufuatana na msemaji wa afisi ya rais wa Kenya, Rais Kiir aliwambia marais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Yoweri Museveni wa Uganda mjini Nairobi jana usiku kwamba atakuwa na mazungumzo ya amani na mhasimu wake mkuu.
Rais Kir alikwenda Nairobi siku ya Ijuma kwa mkutano wa kikanda juu ya miundo mbinu, kuhusu miradi ya ujenzi wa barabara kuanzia Juba hadi lamu na barabara kuu kutokea Mombasa hadi Bujumbura.
Kiongozi huyo wa Sudan Kusini alikutana na rais Kenyatta Jumamosi asubuhi na kumeleza juu ya mazungumzo yake na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry mjini Juba siku ya Ijuma.
Rais Kenyatta, anaeongoza Jumuia ya Ushirikiano wa Serikali ya Afrika Mashariki na Pembe mwa Afrika IGAD, kwa wakati huu, alieleza wazi kwamba Jumuia hiyo haitokubali kuvunjika vunjika kwa mazungumzo yanayoendelea ya kutafuta amani kwa wakati huu.
No comments
Post a Comment