Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, May 28, 2014

HALI YA MUIMBAJI DEBORAH JOHN SAID BAADA YA KUFANYIWA UPASUAJI


Bi Deborah John Said, baada ya kufanyiwa upasuaji wenye mafanikio. ©John Bagenyeka/fb

Hospitali ya Mwananyamala kwenye jengo jipya ghorofa ya kwanza na wodi namba 3 ndio chumba ambacho muimbaji wa nyimbo za injili, Deborah John Said amelazwa, mara baada ya kufanyiwa upasuaji wenye mafanikio na kuondolewa uvimbe uliokuwa unamsumbua.
Taarifa ambazo GK imekuwa ikizipata kuanzia mchana wa leo ni kwamba hali yake inaendelea vizuri, na picha ya mwisho ni ambayo amepigwa baada ya upasuaji. Kwa sasa wamemuacha akiongezewa damu na maji kwa ajili ya kuimarisha afya yake.
Hakika hata sasa Mungu yuko anaendelea kudhihirika kwa kuwa naye katika hatua zote, na Neno ulilotamka juu ya afya ya mtumishi huyu imetimia. Tunasubiri arejee kusimama kwa hali yake na kuendelea kulisifu jina lake BWANA Yesu, yeye aliye juu. Utukufu na umuendee Yesu.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment