Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, May 28, 2014

BABA AMUUA KWA MAWE BINTIYE MJAMZITO KWA KOSA LA KUOLEWA NA ASIYEMTAKA

Mwili wa marehemu Farzana ukiwa chini pembeni yakiwa matofali yaliyotumika kumshambulia.

Wakati Meriam anasubiri kutekelezwa kwa adhabu yake kifungoni huko nchini Sudan, habari nyingine kutoka nchini Pakistan zinasema polisi nchini humo wamemkamata baba mmoja kwa kosa la kumuua binti yake wa kumzaa kwa mawe akishirikiana na familia nzima yenye jumla ya watu takribani 20 kwa kosa la binti yake kuolewa na mwanaume asiyetakiwa na familia.

Marehemu ametambulika kwa jina la Farzana Parveen (25) inadaiwa alikuwa mjamzito wa miezi mitatu wakati ambao kaka zake, baba yake na ndugu wengine walipowashambulia kwa mawe yeye na mumewe aitwaye Mohammad Iqbal (45) majira ya mchana mbele ya mahakama kuu ya mjini Lahore nchini humo.

Kwa mujibu wa mwanasheria na mwanaharakati wa haki za binadamu mkazi wa Pakistani aitwaye Zia Awan amesema hajawahi kusikia aina ya kesi kama ya Farzana kupigwa mawe hadi kifo, mbaya zaidi tukio hilo limefanyika mbele ya mahakama amesema Zia akizungumza na The Associated Press. Naye kwa upande wa baba mzazi wa marehemu Mohammad Azeem ambaye amemfungulia kesi mwanaume aliyefunga ndoa na binti yake bila ridhaa yake licha ya kwamba walikuwa wachumba kwa miaka kadhaa, ameonyesha kutojutia kitendo alichokifanya "Nimemuua binti yangu kwakuwa ameidhalilisha familia nzima kwakuolewa na mwanaume ambaye hakuwa na ridhaa yetu, sijutii kitendo nilichokifanya" amesema mzee Azeem.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa shirika la habari la AP linasema kumekuwa na vitendo vya adhabu za
Mume wa marehemu akiwa na mwili wa mkewe kwenye gari la wagonjwa.
kupigwa mawe katika taifa hilo la kiislamu la Pakistan kwasehemu kubwa kutokana na wanawake kutaka kuolewa kutokana na upendo ama mapenzi kwa ampendaye bali kwa kuchaguliwa mtu wa kuolewa naye jambo ambalo baadhi ya wanawake hawalitaki na kujikuta wakipoteza maisha namna hiyo.
Na katika kuonyesha kwamba vitendo hivyo haviwezi kuisha ni kutokana na adhabu nyepesi wanazopewa watu wanaokamatwa kwa kosa la kuua wenzao kwa kuwarushia mawe. Aidha Awan amesema linapotokea jambo kama hilo polisi hawafanyi uchunguzi kwa makini na kusababisha mahakama kutoa adhabu nyepesi kwa watuhumiwa.

Mapema mwezi wa April, wanandoa wa Kikristo nchini humo walihukumiwa kifo kwakosa la kuukashifu uislamu kwakupitia ujumbe wa simu za mkononi. Licha ya mwanasheria aliyekuwa akiwatetea wanandoa hao kwamba ujumbe huo haukutoka kwao kwakuwa hawajui kusoma wala kuandika lakini utetezi wake haukusikilizwa. Wakristo huishi katika matatizo mazito nchini Pakistani kwakufuatiliwa na polisi, kupelekwa vifungoni na wengine kuhukumiwa kifo.

CP imeandika.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment