Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, April 22, 2014

Waasi wa Sudan Kusini wakana mauaji

Waasi wa Sudan Kusini wamekana mauaji ya raia kwa misingi ya ukabila
Waasi nchini Sudan Kusini wamekanusha madai yaliyotolewa na Umoja wa Mataifa kuwa waliwaua watu kwa misingi ya ukabila.
Msemaji wa waasi, Brigedia Lul Ruai Koang, ameambia BBC kuwa wanajeshi wa serikali ndio waliowaua raia walipokuwa wanaondoka mji wa Bentiu uliotekwa wiki jana na waasi wanaomuunga mkono makamu wa zamani wa Rais Riek Machar.
Jeshi la Sudan Kusini linasema kuwa linakabiliana vikali na waasi hao katika majimbo matatu nchini Sudan Kusini.Umoja wa Mataifa katika ripoti yake iliyotolewa Jumatatu, ulisema kuwa takriban watu miambili waliokuwa wamepewa hifadhi msikitini na wengine wengi wakiwa wanahifadhiwa hospitalini na makanisani waliuawa kwa sababu ya kabila lao.
Zaidi ya watu milioni moja wamelazimika kuondoka makwao tangu mapigano kuanza Disemba mwaka jana.
Mgogoro huo ni kati ya Rais Salva Kir wa kabila la Dinka na Riekl Machar aliyekuwa makamu wa Rais anayetoka kabila la Nuer
Pande zote mbili zinasemekana kufanya mauaji.
Lakini mauaji yaliyofanywa na waasi mjini Bentiu, Bor na Malakal, umewafanya watu kumchukia kiongozi wa waasi Riek Machar.
Mapigano huenda yakaanza tena ingawa pia mazungumzo ya kusitisha vita yanatarajiwa kuanza nchini Ethiopia katika wiki chache zijazo.
Kumekuwa na taarifa za jeshi kuwalenga watu wa kabila la Nuer huku waasi wakiwalenga watu wa jamii ya Dinka.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment