Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, April 5, 2014

‘Tukirudi Bungeni, katiba tayari’

Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Tundu Lissu (katikati) Ismail Jussa (kushoto) na Ibrahim Sanya wakibadilishana mawazo kwenye Viwanja vya Bunge hilo, mjini Dodoma. Picha na Silvan Kiwale. 
Na Editha Majura, Mwananchi
Mwenyekiti wa Ukawa na Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Freeman Mbowe, amesema kuna kila dalili watakaporudi bungeni hatima ya mchakato wa Katiba Mpya ya Tanzania utakuwa umeiva.
Mbowe ambaye pia ni kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani katika la Bunge la Jamhuri ya Muungano, alilieleza gazeti hili kuwa hali hiyo inatokana na yanayoendelea kwenye vikao vya Kamati za Bunge.
Kauli ya Mbowe ilitolewa muda mfupi kabla viongozi wa Ukawa hawajaanza kikao kilicholenga kutathmini vikao vya Kamati za Bunge Maalumu vilivyoanza Jumatatu wiki hii.
Awali, kulikuwa na taarifa za kuvunjika kwa Bunge hilo kulikoelezwa kupangwa na Ukawa kwa kilichodaiwa kuwa ni kuchoshwa kuburutwa na CCM. Hata hivyo taarifa hizo zilikanushwa. Mara ya mwisho madai hayo yalikanushwa na Kaimu Mwenyekiti wa Ukawa, John Mnyika alipozungumza kwa niaba ya Mbowe bungeni wakati akielezea mwafaka wa mjadala wa matumizi ya kura ya wazi au siri katika kupitisha vipengele vya rasimu.
Alisema taarifa zilizoelezwa kuwa Ukawa wamekusudia kuvuruga mchakato huo hazikuwa na ukweli wowote na kwamba wangekuwa wa mwisho kutaka kufikia uamuzi huo.
Lakini ratiba ya utekelezaji majukumu ya Bunge kupitia kamati ilipotolewa na kuelekeza kuwa mijadala itaanza kwa kushughulikia sura ya kwanza na sita ya Rasimu ya Pili, baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo akiwamo Mbunge Arusha, Godbless Lema walitangaza kujiondoa.
Hata hivyo, umoja huo ulitoa msimamo wake kuwa wanashiriki kuboresha sura ya kwanza na ya sita ya rasimu, lakini hali ya ukiukwaji wa kanuni ikiendelea, watalazimika kuchukua uamuzi mazito.
Taarifa kutoka ndani ya baadhi ya kamati, zinasema baadhi ya wajumbe wenye msimamo wa serikali mbili wamekuwa wakiingia na kulazimisha kuingiza maoni yenye msimamo huo.
Miongoni mwa kamati hizo ni pamoja na ya sita, inayoongozwa na Stephen Wassira, ambaye mpaka jana hakuwa ametoa taarifa rasmi ya mambo yanavyoendelea ndani ya kamati yake kwa vyombo vya habari.
Akizungumza kwa simu na gazeti hili, Wassira alisema mambo yalikuwa yakiendelea vizuri na kwamba angetoa taarifa rasmi leo.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment