Writen by
sadataley
4:47 PM
-
0
Comments
Miili ya watu sita ambao walifariki dunia baada ya kupigwa risasi na watu wasiofahamika takribani wiki mbili zilizopita katika kanisa la Joy in the Lord huko Likoni mjini Mombasa nchini Kenya imesafirishwa kuelekea kwa ndugu zao tayari kwa mazishi baada ya ibada fupi iliyofanyika jana asubuhi na kuhudhuriwa na kamanda wa polisi wa Mombasa Nelson Marwa.
Katika ibada hiyo kamanda Marwa aliwataka vijana kutojiingiza katika vitendo vya kigaidi kwakuwa watakabiliwa na nguvu za jeshi. Katika tukio hilo lililotokea wiki mbili zilizopita lilishuhudia risasi ikituhama kichwani kwa mtoto mdogo wa mwaka mmoja na nusu aitwaye Satrine Osinya ambaye madaktari wa hospitali kuu ya Kenyatta jijini Nairobiwalifanikiwa kumtoa risasi hiyo kwasasa anaendelea kutibu jereha hilo la kichwa.
Mtoto Satrine wakati akifanyiwa upasuaji hivi majuzi hospitali ya Kenyatta jijini Nairobi. |
Habari na picha kwahisani ya NTV Kenya.
No comments
Post a Comment