Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, April 22, 2014

Mbowe: Hakuna aliyemtusi Mwalimu Nyerere, wala anayetaka kuvunja Muungano

Mwenyekiti wa Umoja wa Katiba ya Watanzania (Ukawa), Freeman Mbowe, amesema uamuzi wao wa kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge ni sahihi kwa kuwa ni njia ambayo imeonekana kwao kuwa inafaa kudai haki ya Watanzania wote.
Mbowe ambaye pia ni kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alisema hayo muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa ndani wa Ukawa.
Mkutano huo pamoja na mambo mengine ulijadili mikakati mbalimbali inayohusu umoja huo ambao sasa wanapeleka masuala yao kuhusu mchakato wa Katiba Mpya kwa wananchi.
Ukawa pamoja na baadhi ya wajumbe wa Bunge la Katiba kutoka kundi la 201, walitoka nje ya Ukumbi wa Bunge mjini wakidai kutoridhishwa na mwenendo wa Bunge hilo lenye lengo la kutengeneza Katiba Mpya.
“Kuendelea kushiriki mchakato huu, ni kuubariki na kuupa uhalali udhalimu unaoendelea ndani ya Bunge Maalumu, hatuwezi kushiriki mjadala wenye matusi, kejeli, dharau na unaopotosha umma, kwa kupindisha kauli zilizowahi kutolewa na viongozi wetu,’ anaeleza Mbowe.
Mbowe anasema wajumbe wa upande wao kila walipotoa mtazamo wao, wakieleza ukweli, wajumbe wa upande wa pili wanapopata nafasi ya kuchangia mjadala badala ya kutoa mapendekezo yao na kuyatetea kwa hoja, wanageuza ukweli wa maoni yaliyotolewa na wale wa upande wa Ukawa, anasema ni karaha ambayo ni vigumu kuielezea ikaeleweka.
Akahoji wanaodai wamekosea kujitoa katika mijadala hiyo ikiwa wanafurahishwa na udhalilishaji ambao wamefanyiwa tangu kuanza mjadala unaohusu sura ya kwanza na sita za Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya.
Anataka pia watu wajiulize, je kwa mchakato wa aina hii kitapatikana kile wanachotaka? Anasema kazi yao kama vyama vya siasa ni kuweka shinikizo na kujenga hoja zenye kushinikiza kupatikana kile kinachohitajika kwa masilahi ya taifa.
Anasema hawawezi kuwa sehemu ya mijadala inayopuuza maoni ya wananchi ambayo yamepatikana kwa kukusanywa na chombo (Tume ya Mabadiliko ya Katiba) kilichoundwa na serikali na kufanya kazi kwa mujibu wa sheria iliyoidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Mbowe anabainisha kuwa baada ya kubaini kutokuwapo uwezekano wa kubadili nyendo za wenzao bungeni, wakaafikiana kuwa kinachofuata ni kuunda busara yoyote ambayo wanaweza kuitumia kuokoa taifa dhidi ya genge la watu kama wale, ambao wamekaririshwa maneno.
“Wao wanatulaumu Ukawa tunaweka misimamo, lakini wao wanakuja na mambo ambayo wameyajadili katika mikutano yao ya ndani na Waziri Mkuu akiwa miongoni mwao. Wanaweka mikakati ya kuzomea, watu wanazomewa pale, kauli za utenganisho zinatajwa na watu wanashangilia bila kujali kuwa wanapasua taifa - hatuwezi kuendelea kuwa sehemu ya wapasua taifa,” anasema Mbowe.
Anasema wameamua kwenda kwa wananchi kuwaambia kinachoendelea bungeni, wao ndiyo wataamua anasema kadhalika waliobaki siku za usoni wanaweza wakapata busara wakaona kuwa kutunga Katiba peke yao ni jambo lisilo na uhalali.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment