Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, April 5, 2014

3 wahukumiwa kifo kwa ubakaji India

Wanaume watatu wamehukumiwa kifo Mjini Mumbai, India baada ya kupatikana na hatia katika visa tofauti vya ubakaji walioufanya kwa pamoja.
Maandamano ya kupinga ubakaji India
Moja ya visa hivyo kilitokea dhidi ya mwandishi mpiga picha aliyekuwa kazini alipobakwa.
Sheria hiyo ilipitishwa baada ya kile kisa Delhi kilichoughadhabisha umma cha msichana aliyebakwa na ngege basini na kujeruhiwa vibaya sana.Uamuzi huo umefanywa chini ya sheria mpya iliyopitishwa ya kuwaadhibibu wanaoendeleza uhalifu huo wa ubakaji.
Wanaume hao walikuwa wameshitakiwa kwa kesi ya kumbaka msichana huyo mwandishi aliyekuwa ameenda kupiga picha kiwanda cha nguo kilichotelekezwa, lakini pia mwanamke mwengine akajitokeza na kutoa ushahidi wa jinsi wanaume hao walivyombaka maeneo hayo hayo mwezi mmoja kabla.
Wahukumiwa hao wanaweza kukata rufaa kwa mahakama ya juu zaidi.
Kuongezaka kwa visa vya ubakaji vimepelekea maaandamano ya mara kwa mara nchini humo na sasa mahakama zinaharakisha kusikilizwa kwa kesi hizo.
Pia limekuwa swala la mijadala mikali katika kampeni za uchaguzi unatajariwa hivi karibuni nchini humo.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment