Writen by
sadataley
3:24 PM
-
0
Comments
Rais wa World Vision Richard Stearns.©Mtlmagazine |
Baada ya Rais huyo kutangaza hatua ya shirika hilo taarifa ambayo imezua mkanganyiko miongoni mwa viongozi maarufu wa Kikristo ambao makanisa yao pamoja na taasisi hutoa misaada katika shirika hilo wakitaka makanisa na viongozi kususia uamuzi wa shirika hilo kwakuwa kwakuruhusu watu wanamna hiyo kufanya kazi ndani ya shirika hilo ni kwenda kinyume na neno la Mungu ambalo linapingana na vitendo vya mapenzi kwa watu wenye jinsia moja.
Katika taarifa mpya hapo jana Rais wa World Vision Richard Stearns hakuwa na jinsi zaidi ya kuomba msamaha kwa watu wote na viongozi wa makanisa mbalimbali ambao wamehuzunishwa ama kukwazwa na hatua iliyotaka kuchukuliwa na shirika hilo, na kutokana na mkanganyiko huo uliojitokeza shirika hilo limefuta kauli yake ya kutaka kuwaajili watu hao.
Lakini wakati Rais huyo akibadili uamuzi wa shirika hilo, tayari mwenyekiti wa makanisa ya Assemblies of God duniani George Wood amelitaka kanisa hilo pamoja na waumini wake ambao wamekuwa wakilisapoti shirika hilo, kuacha kufanya hivyo kwakuwa kanisa lao na mengine ya Kipentekoste yanafundisha kwakufuata Biblia.
No comments
Post a Comment