Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, February 2, 2014

Wasaliti na wakaidi CCM sasa basi, asema Kanali Kinana

Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana 
Na Lauden Mwambona, Mwananchi
Mbeya. Chama Cha Mapiduzi (CCM), kimetishia kuwatimua mara moja, wanachama wasaliti na wasiokubali kushindwa wakati wa kura za maoni za kuwania kuteuliwa ili kugombea urais, ubunge na udiwani.
Tishio hilo lilitolewa jana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Kata ya Nsalaga jijini Mbeya.
Kiongozi huyo mtendaji wa CCM alikwenda katika eneo hilo kukagua kazi za maendeleo ukiwemo ujenzi wa Ofisi ya CCM ya kata inayojengwa kwa nguvu za wanachama.
Kinana alisema Kata ya Nsalaga ina diwani wa upinzani na kwamba hiyo imetokana na CCM kukosea kuteua mgombea asiyetakiwa na wapigakura.
Alisema sababu nyingine ni usaliti unaotokana na walioshindwa katika kura za maoni ya kuwania kuteuliwa kuwa wagombea.
“Wasaliti walio CCM sasa basi, hawatavumiliwa na watakaogundulika tutawaonyesha njia ya kwenda wanakotaka,’’ alisema.
Kuhusu ujenzi wa Ofisi ya CCM, Kinana aliwapongeza wananchi wa kata hiyo kwa kujenga ofisi kuu.
Maadhimisho hayo yanafanyika leo jijini hapa ambapo asubuhi hii, Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete aliyetarajiwa kuwasili jana jioni, anatazamiwa kuongoza matembelezi ya mshikamano yatakayoanzia eneo la Soweto hadi Uwanja wa Sokoine.
Kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, Rais Kikwete atawahutubia wanachama wa CCM katika Uwanja wa Sokoine baada ya matembezi hayo ya maadhimisho.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment