Writen by
sadataley
2:56 PM
-
0
Comments
Na Geofrey Nyang’oro na Berdina Majinge, Mwananchi
Iringa.Wagombea wanne wa Ubunge Jimbo la Kalenga kupitia Vyama vya CCM, Chadema, NCCR-Mageuzi na Causta jana wamerejesha fomu za kuwania kiti cha ubunge wa jimbo hilo baada ya kukamilisha taratibu za kujaza fomu, huku wale wa CCM na Chadema wakitoa ujumbe mzito wa kuwataka wafuasi wa vyama vyao kutojihusisha na vurugu wakati wa kampeni.
Kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo unaotarajiwa kufanyika Machi 16 mwaka huu na kampeni zinaanza kutimua vumbi leo kwa mujibu wa ratiba ya jumla iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi Taifa (NEC). Kampeni zitadumu mpaka Machi 15 mwaka huu.
Wagombea waliorejesha fomu jana ni pamoja na Godfrey Mgimwa (CCM) Grace Tendega (Chadema) Erick Chelula NCCR-Mageuzi na Richard Minja (Chausta).
Baada ya kurejesha fomu hizo katika Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Pudenciana Kisaka, aliwapongeza kwa hatua waliyofikia na kuwatakia kila la heri katika kampeni zao.
No comments
Post a Comment