Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, February 18, 2014

Vita vyazuka tena Malakal, Sudan.K

Haya ni mapigano ya kwanza tangu kutia saini mkataba wa kusitisha vita
Mapigano yanaripotiwa kuzuka Sudan Kusini kwa mara ya kwanza tangu serikali na waasi kutia saini makubaliano ya kusitisha vita mwezi Januari.
Waasi wanaomtii makamu wa Rais wa zamani Riek Machar, wameshambulia mji wa Malakal, ambao ni mji mkuu wa jimbo la Upper Nile linalozalisha mafuta kwa wingi.
Majeshi ya serikali, yamepambana vikali na waasi hao katika maeneo tofauti ya mji huo.
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa mjini Juba, (Toby Lanzer), amezitaka pande zote kwenye mzozo huo, kulinda raia.
Makabiliano hayo bila shaka yanazua wasiwasi kuhusu hali ya usalama katika visima vya mafuta Kaskazini mwa nchi. Mafuta ya Sudan Kusini ndio uti wa mgongo wa uchumi wa nchi hiyo
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment