Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, February 24, 2014

Urusi watawala Olimpiki Sochi

Mashindano yakamilika Sochi
Makala ya 22 ya Michezo ya Olimpiki ya msimu wa baridi yalikamilika jumapili mjini Sochi Urusi baada ya siku 17 ya mashindano.
Mashindano hayo yaligharimu dola bilioni 30, ambayo ni kitita kikubwa zaidi katika historia ya mashindano ya Olimpiki duniani IOC.
Alisema wanaondoka Sochi wakiwa marafiki bila ya kumbukumbu ya changamoto zilizokuwepo awali.Rais wa shirikisho la Olimpiki duniani (IOC) Thomas Bach aliirai dunia kuitizama Urusi kwa mtazamo mpya kwani wamezidisha matarajio ya washiriki wengi walioshiriki mashindano ya msimu wa baridi Sochi.
Sherehe za kufunga mashindano Sochi



Bach Alisema Urusi aliyoiona katika mashindano ya msimu wa baridi huko Sochi ni taifa jipya na karimu mno.
Zaidi ya wanariadha 2800 kutoka mataifa 88 walishiriki katika mashindano hayo yaliyojumuisha michezo 12 mpya .
Urusi ilimaliza ya kwanza katika jedwali la medali ,ikiwa na medali 13 za dhahabu 11 za fedha na 9 za shaba.
Norway ilimaliza ya pili na medali 11 za dhahabu 5 fedha na 10 za shaba.
Canada ilikamilisha orodha ya tatu bora na jumla ya medali 10 za dhahabu 10 za fedha na 5 za shaba.
Baada ya kuandalia dunia dhifa ya kukata na shoka waandalizi wa mashindano ya Sochi waliwakabidhi wenzao kutoka Korea kusini bendera ya kamati ya olimpiki .

Mji wa Pyeong-chang ulioko Korea Kusini ndio utakaokuwa mwenyeji wa mashindano yajayo ya olimpiki ya msimu wa baridi mwaka wa 2018.

Jedwali la Medali Sochi

 Taifa           Dhahabu          Fedha              Shaba 
1 Urusi          13                           11                       9 
2 Norway      11                           5                     10 
3 Canada      10                         10                      5 
4 Marekani     9                        7                     12 
5 Uholanzi      8                        7                       9 

Chanzo:bbc swahili
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment