Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, February 1, 2014

Upinzani watatiza uchaguzi Thailand

Waandamanaji nchini Thailand wanazuia usambazaji wa karatasi za kupigia kura siku moja tu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu unaosusiwa na upinzani.
Maandamano yanayotatiza mchakato wa uchaguzi Thailand
Makundi ya waandamanaji wanaopinga serikali yalizingira ofisi moja ya serikali katika mji mkuu wa Bangkok ,ambapo karatasi za kupigia kura katika zaidi ya vituo 100 zimewekwa.
Karatasi kama hizo pia zimezuiliwa katika ngome ya upinzani kusini mwa taifa hilo.
Upinzani unataka kuondolewa kwa kile inachokitaja kama serikali fisadi ya waziri mkuu Yingluck shinawatra ambaye wamekuwa wakidai ni kibaraka wa kakaake mkubwa Thaksini Shinawatra.
Thailand inajiandaa kwa uchaguzi mkuu siku ya Jumapili,licha ya upinzani kuususia na hata kutatiza maandalizi yake. Inaarifiwa huenda bwana Yingluck shinawatra akachaguliwa tena, kitu kinachowaudhi wapinzani.
Mamia ya waandamanaji walipiga kambi katika vituo vya kusambazia karatasi za kupigia kura mjini Bangkok ili kuzuia shughuli ya kusambaza karatasi hizo kabla ya uchaguzi mkuu Jumapili.
Polisi walijitahidi kuwatawanya wafuasi wa serikali na wapinzani baadhi waliokuwa wamejihami kwa vijiti na vyuma huku hali ya taharuki ikitanda mjini Bangkok.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment