Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, February 20, 2014

Ujerumani : Raia wa Rwanda Onesphore Rwabukombe ahukumiwa kifungo cha miaka 14 jela

Onesphore Rwabukombe na wakili wake, januari 18 mwaka 2011, mjini Frankfurt
Onesphore Rwabukombe na wakili wake, januari 18 mwaka 2011, mjini Frankfurt
Daniel Roland. AFP

Na RFI
Mahakama moja mjini Frankfurt nchini Ujerumani imemuhukumu kwa mara ya kwanza jana raia wa Rwanda aliekutikana na hatia ya kushiriki katika mauaji ya kimbari yaliyosbabisha mamia kwa maelfu ya raia kupoteza maisha kati ya aprili na julai mwaka 1994.

Onesphore Rwabukombe, mwenye umri wa miaka 56, amepewa adhabu ya kifungo cha miaka 14 jela, baada ya ya mashuhuda 120 kusikilizwa na kutoa ushuhuda wao, huku kukiwa kulioneshwa filamu nyingi ambazo zilimuonesha Onesphore Rwabukombe, akihusika katika mauaji hayo.
Ofisi ya masitaka iliku ilimuombea Onesphore Rwabukombe kifungo cha maisha jela, lakini upande wa utetezi walikua wameomba mteja wao aachiwe huru, wakibaini kwamba hana hatia.
Rwabukombe, meya wa zamani wa wilaya ya Muvumba, kaskazini mashariki mwa Rwanda, alihukumiwa baada ya kukutwa na hatia ya kuamuru wanajeshi, askari polisi na wanamgambo wa kihutu, Interahamwe, kutoka chama tawala cha zamani cha rais Juvenal Habyarimana (MRND) kutekeleza mauwaji ya mamia ya watu kutoka jamii ya watutsi waliyokua walipewa hifadhi katika kanisa moja kijijini Kiziguro.
Amekuwa akiishi kama mkimbizi wa kisiasa nchini Ujerumani tangu mwaka 2002.
Serikali ya Rwanda imepongeza uamuzi wa mahakama ya Frankfurt, Nchini Ujerumani kumhukumu Aliyekuwa meya wa zamani nchini Rwanda, Onesphore Rwabukombe, kifungo cha miaka 14 jela baada ya kushukiwa kwa makosa ya kushindwa kuzuia mauaji ya Rwanda mwaka 1994.
Rwanda inasema pamoja na kwamba kesi hiyo imesikilizwa nje ya nchi ni ishara kwamba sheria za kimataifa zinaheshimiwa popote pale mshukiwa anapokimbilia.
Mawakili wa Rwabukombe, wamesema watakata rufaa.
Rwabukombe, alikamatwa tangu mwaka 2011, baada ya Rwanda kutoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.
“Ujerumani si hifadhi ya watu waliyoshiriki katika mauaji ya kimbari (...), tumeridhishwa na jinsi kesi hii ilivyoendeshwa, muendesha mashitaka mkuu Christian Ritscher, ameiamba AFP.
Mataifa ya Ulaya yamekua yakishuhulikia kesi za watu wanaotuhumiwa mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda.
Hivi karibuni mahakama nchini Ufaransa ilianza kusikiliza kesi inayomkabili raia mwengine wa Rwanda, Pascal Simbikangwa, mbaye anatuhumiwa kuhusika katika mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda mwaka 1994.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment