Writen by
sadataley
6:02 PM
-
0
Comments
Vatican. Katika hotuba yake ya kila siku, Papa Francis alizungumza kuhusu umuhimu wa kuwa wanafunzi wa Kristo , na kusisitiza haja ya Wakristo kumfuata Yesu kwa maisha yao yote, si tu kielimu ." Yesu hakusema kwa Petro na wenzake 'mnanijua mimi! " Alisema ,' Nifuate aliendelea kuelezeaa juu ya uhusiano wa Petro pamoja na Yesu katika Injili.
Alizungumzia pia jibu la Petro kwa swali la Yesu, " Na ninyi je, husema kwamba mimi ni nani? "
" Petro alikuwa jirani sana na Yesu , aliona miujiza ambayo Yesu alifanya , aliona uwezo wake ... lakini katika hatua fulani , Peter alimkataa Yesu," alieleza Baba Mtakatifu .
Kupitia uzoefu huu, Petro alijifunza " hekima - . Kwamba kilio kile cha machozi mengi sana alicholia. Kama Petro , kila Mkristo lazima kujifunza " kumfuata Yesu katika nguvu yetu, na hata katika dhambi zetu, lakini tunapaswa kumfuata Yesu siku zote."
Njia ya uanafunzi hauzuii maarifa na akili ,"Ni muhimu kujifunza na kujua" mambo kama katekisimu. Alisema kwamba maarifa peke yake " si ya kutosha. " Badala yake, kile ambacho ni muhimu ni "mkutano wa kila siku na Bwana, kila siku , na ushindi wetu na udhaifu wetu."
"Mara nyingi , Yesu anarudi kwa sisi na anauliza, ' lakini mimi ni nani kwa ajili yenu? " Alisema Papa. Ili si kujibu tu " kama ambavyo tumejifunza katika katekisimu ," tunapaswa kutambua mahitaji yetu kwa msaada wa Mungu .
"Ni kwa muda tu tunapaswa kuwepo katika maisha ya kikristo " katika safari hiyo hatuwezi kufanya peke yake." Badala yake , hatuna budi kurejea na kupata msaada zaidi katika udhihirisho ule wa Mungu kwetu yaani Baba, Mwana na Roho Mtakatifu(Trinity).
"Ili kujua Yesu ni zawadi ya Baba, naye alituwezesha sisi kumjua Yesu. Ni kazi ya Roho Mtakatifu , " alisisitiza Papa Francis.
Aidha, Roho Mtakatifu ni kiunganishi mratibu wetu , hufanya kazi na huishi nasi siku zote. Anafanya kazi hii kwa kufunua huduma ya Yesu " katika maisha yetu.
Kisha Papa aliutaka mkutano kufikiria wito wa kufanya Injili katika maisha yao binafsi.
" Hebu tumuangalie Yesu, Petro na mitume wengine na tujiulize katika mioyo yetu swali hili : ' Yesu ni nani kwetu sisi"
"Kama wanafunzi , hebu tujiulize kwanini Baba ametupa maarifa haya kwa njia ya Kristo katika Roho Mtakatifu, " alihitimisha.
Makala hii imetafsiriwa nami Mchungaji Kurwa Sadataley
toka http://www.catholicnewsagency.com/news/to-know-jesus-we-must-follow-him-says-pope-francis
No comments
Post a Comment