Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, February 3, 2014

Mali ya hayati Mandela yatangazwa

Hayati Nelson Mandela, aliachia familia yake mali yake yenye thamani ya dola milioni 4.1
Mandela alifariki mwezi Disemba mwaka jana akiwa na umri wa miaka 95
Sehemu ya mali hiyo pia itatolewa kwa chama tawala ANC, wafanyakazi wake wa zamani na shule kadhaa ambako alisomea.
Afisaa Dikgang Moseneke aliyekabidhiwa jukumu la kusoma wasia huo wenye kurasa 40 na kuhakikisha unatekelezwa ,alisema hapajakuwa na pingamizi zozote kuhusu yaliyomo kutoka kwa familia ya Mandela.Hayo ndio yalikuwa mapenzi ya Mandela ambayo yalikuwa kwenye wasia wake uliosomwa hadharani kwa familia nzima.
Wafanyakazi wa karibu wa Mandela watapata randi 50,000 kila mmoja. Shule ambazo Mandela alisomea zitapata randi laki moja kila shule.
Hayati Mandela alifariki akiwa na umri wa miaka 95.
Familia ya Mandela tangu hapo imekuwa ikizozana kuhusu urithi wa hayati Mandela na kuna hofu kuwa huenda wasia huu ukasababisha mgogoro mwingine kuhusu mali hiyo.
Mali ya hayati Mandela inajumuisha nyumba na hakimiliki za vitabu ikiwemo kimoja kuhusu maisha yake kwa jina ''Long walk to freedom''
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment