Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, February 18, 2014

Maaskofu wakataa ushoga Uingereza


Alama ya kanisa, msalaba 

London. Maaskofu wakuu nchini Uingereza wamewaambia viongozi wa dini kwamba hawataruhusiwa kuingia katika ndoa za jinsia moja.
Pia walisema kwamba hawatakubali kuona viongozi wa dini kwenda kinyume na maagizo hayo nchini humo.
Viongozi wa dini wa kanisa la Ki-Anglikana wanakubaliwa na kanisa hilo kuingia katika uhusiano wa kimapenzi lakini kwa maelewano kwamba hawatashiriki ngono.
Katika mwelekeo wao, maaskofu hao pia walipiga marufuku maombi yoyote maalumu kwa wanandoa wa jinsia moja licha ya ripoti rasmi ya kanisa hilo kupendekeza kwamba viongozi wa dini wanaweza kufanya hivyo iwapo wanajihisi.
Hata hivyo walidai viongozi wa dini wanapaswa kutoa maombi yasiyo rasmi kwa wanandoa walio katika uhusiano wa jinsia moja.
Uganda
Kwa upande wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda alisema atasaini muswaada tata unaopinga ushoga na kuwa sheria kamili.
Hatua hiyo inaelezwa kuwa ni onyo kwa wanaotetea vitendo vya mahusiano ya jinsia moja kuwa watashughulikiwa vikali nchini humo.
Mwezi uliopita kiongozi huyo alipanga kuachana na mswada huo ambao umekuwa ukikosolewa vikali na wahisani kutoka mataifa ya Magharibi na wanaharakati wa haki za binaadamu tangu ulipowasilishwa mwaka 2009.
Mapenzi ya jinsia moja ni mwiko katika mataifa ya Afrika na kinyume cha sheria kwa mataifa 37.
Wasiwasi wa mashoga wa Afrika
Wanaharakati wa haki za binaadamu wanasema Waafrika wachache waliojitangaza kuwa mashoga, wanahofu ya kufungwa, kukabiliwa na vurugu na kupoteza ajira zao.
Wakati wa mkutano wake na chama tawala nchini Uganda NRM kundi la wanasayansi liliwasilisha utafiti wao kuhusu mapenzi ya jinsia moja kwa Rais Museveni.
Msemaji wa mkutano huo, wa NRA Anite Evelyn katika taarifa yake alisema kuwa “Museveni alitangaza atasaini mswada huo kwa vile swali lile la iwapo mtu anaweza kuzaliwa shoga au hapana limejibiwa”.
Uchunguzi wa mawaziri
Katika taarifa yake kamati ya mawaziri iliyokuwa ikilifanyia uchunguzi suala hilo ilisema hakuna vinasaba vya mapenzi ya jinsia moja na kwa hivyo si ugonjwa lakini ni tabia isiyo ya kawaida ambapo mtu anaweza kujifunza tu kwa kupitia uzoefu katika maisha.
Katika mkutano na chama tawala cha NRM, Mshauri wa Rais katika masuala ya Kisayansi, Dokta Richard Tushemereirwe alimwambia kwamba “mapenzi ya jinsia moja yana athari kubwa kwa afya za watu kwa hivyo si jambo la kuachwa liendelee hata kidogo”.
Mswada wa kupinga uhusiano wa jinsia moja uliwasilishwa bungeni mwaka 2009, ambapo awali ulikuwa ukipendekeza adhabu ya kifo kwa wanaoshiriki vitendo vya ngono kwa watu wa jinsia moja, lakini ukafanyiwa marekebisho kwa kuweka adhabu ya vifungo vya awamu gerezani na maisha kwa kile kilichotajwa kuwa mapenzi ya jinsia moja ya kuchochewa.
Rais Museveni alisisitiza kuwa , wahamasishaji, wanaojionesha na wote wanaoshiriki vitendo vya ngono kwa watu wa jinsia moja kwa sababu za ukaidi wa kutumwa , hawatavumiliwa na watakabiliwa vikali
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment