Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, February 4, 2014

Kundi la Taleban laondoka mazungumzoni

Wawakilishi wa kundi moja la wapiganaji wa Taleban nchini Pakistan ambao wako katika mazungumzo ya amani wamekasirika baada ya ujumbe wa serikali kudinda kuhudhuria mazungumzo ya awali.
Taleban yalaumu serikali kwa kuchelewesha mazungumzo
Mjumbe mmoja wa kundi hilo ameitaja hatua hiyo kama njama ya serikali kuchelewesha mazungumzo hayo huku akionya kuwa 'chochote chaweza tokea kwa sasa'.
Awali,wazungumzaji waliokuwa wakiiwakilisha serikali walilitaka kundi hilo kuelezea ni akina nani waliokuwa katika kundi lao.Ujumbe huo tayari umeondoka katika mji mkuu wa Islamabad.
Waandishi wanasema kuna wasiwasi kuhusu matarajio ya mazungumzo hayo kwa kuwa kundi la Taleban linasisitiza kuhusu kuidhinishwa kwa sheria za kiislamu pamoja na kuachiliwa huru kwa wafungwa wote wa Taleban.
Kundi la Taleban kutoka Pakistan lina mchanganyiko wa wanamgambo wa kiislamu wenye itikadi kali ambao wanataka kuanzisha utawala wa kiislamu.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment