Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, February 6, 2014

Kinana: Tunataka CCM ya Nyerere na Karume

“CCM tuliyoachiwa na waasisi wetu ilikuwa ni ya kutetea wanyonge, kuwatetea wazee, watoto, yatima na wajane... Hivyo, CCM ya sasa lazima iwatetee wakulima, wafanyakazi na hata wafanyabiashara wanaoonewa.” Abdulrahman Kinana  
Na Lauden Mwambona, Mwananchi
Mbeya. Wiki hii Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alimpongeza Kinana akisema ameanza kukirudisha chama kwenye mstari.
Kwa kauli yake, Rais Kikwete anasema ‘’Hongera Ndugu Kinana kwa kusimamia na kutekeleza kwa vitendo maazimio ya Mkutano Mkuu wa chama chetu.  Napenda kutumia hii fursa kutoa wito kwa viongozi wote wa chama na ngazi zote kuiga mfano huu mzuri.’’
Maazimio ya Mkutano Mkuu wa mwaka 2012 ni yapi?
Kimsingi maazimio yapo mengi, lakini Mwenyekiti wa CCM anasema ni kama yapo matatu kwa ujumla wake.
Anasema mambo hayo ni kuimarisha CCM kama taasisi, viongozi wa CCM kufanya kazi ya chama kwa kuwa karibu na wananchi na pia kufuatilia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi 2010.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa kwenye ziara ya Mkoa wa Mbeya mwishoni mwa mwaka jana alitangaza waziwazi kwamba yeye anataka CCM ya waanzilishi, yaani ya Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume irudi.
Anasema CCM lazima ipinge unyonyaji, ukabaila uzembe na ufisadi kwa nguvu zote.
Anasema viongozi wa CCM lazima waitishe vikao vyote vya kikatiba kuanzia mashina, matawi, kata, wilaya na mikoa kama ilivyo kwa vikao vya kitaifa.
Viongozi hao wa CCM, Kinana anasema, lazima watoke ndani ya CCM na kusisitiza kwamba makatibu wa mikoa wawe na utaratibu wa kuwapendekeza wanaofanya vizuri kupanda vyeo kuwa makatibu wa wilaya, hali kadhalika wa wilaya lazima wawapendekeze wale wa kata ili wapande vyeo wanaofanya vizuri.
 Anatamka wazi  kwamba hivi sasa mambo mengine ndani ya CCM ni ya ‘hovyo kabisa’ na yanahitaji marekebisho ya haraka.
Kwa mujibu wa Kinana, kama alivyosisitiza Rais Kikwete Jumapili, kuimarisha Chama Cha Mapinduzi ni pamoja na kufanya kazi ya chama ndani ya umma. 
Kwamba viongozi wa chama lazima watoke kwenda kuwatembelea wananchi, kuzungumza nao, kuona au hata kushiriki katika shughuli zao hususan kilimo na ufugaji.
Kwa habari zaidi ingia www.mwananchi.co.tz
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment