Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, February 3, 2014

KILICHOTOKEA DUNIANI KATIKA PICHA

Rais Kikwete, Makamu wa Rais Dk Bilal, na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wkiwa katika picha ya pamoja na Waziri na manaibu waziri mara baada ya kuapishwa, katika hafla fupi iliyofanyika ikulu tarehe 30 2014, hafla hii inafuatia ile ya awali iliyofanyika tarehe 20 ambapo wateule hawa hawakuwepo. ©Ikulu Blog
Rais Kikwete, Mamamu wa Rais Dr Bilal, na Waziri Mkuu Mizengo Pinda pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Sefue wakiwa katika pichaya apmoja na mawaziri na manaibu waziri baada ya kuapishwa kwenye viwanja vya ikulu wiki tarehe 20 Januari. ©Ikulu Blog


Rais Kikwete akizunguma na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Mathias Chikawe baadaya kuapishwa, akiwa na Inspekta Jenerali wa Polisi, Ernest Mangu pamoja na makamishna na maafisa wengine kutoka mamlaka zilizo chini ya wizara hiyo. ©Ikulu Blog


Mafuriko Morogoro;
Maelfu ya watu walijikuta katika hali ngumu mara baada ya mafuriko kutokea Morogoro na viunga vyake; Dakawa, Dumila na Kilosa w takriban kaya 3,000 walikosa walibaki bila makazi baada ya maeneo yao kuharibiwa. Rais Kikwete aliagiza tathmini ya maafa ifanyike upya ili kuhakikisha idadi ya walioathirika ili wapate kusaidiwa mapema iwezeanavyo.
Rais Jakaya Kikwete akikagua ukarabati wa daraja la Mto Mkundi ambalo lilisombwa na mafuriko hivi karibuni na kusababisha magari ya abiria na mizigo kukwama. wakati alipotembelea maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko. ©Freddy Maro/Ikulu Blog


Huko Serbia;
Mtambo wa kusafisha barabara ukiondoa snow ambayo imeziba njia na kusababisha kukwama kw amawasiliano kwenye baadhi ya maeneo nchini Serbia, ikiwemo treni mbili za abiria ambapo mojawapo ilikuwa inatokea Hungary siku ya Jumamosi kutokana na reli kufunikwa kwa mita kadhaa. Mamlaka husika zilizamika kuchukua hatua ya tahadhari kufunga barabara kadha ili kuhakikisha usalama. ©AP




Ukraine;
Licha ya Waziri Mkuu wa Ukraine kujiuzulu kufuatia maandamano ambayo yamedumu kwa takriban miezi mitatu sasa, hali ya Ukraine bado si shwari, kutokana na utofauti wa itikadi za kisiasa na mtazamo wa wananchi juu ya kujiunga na Umoja wa Ulaya (EU), jambo ambalo taifa la Urusi lilijitahidi kusaini mikataba kadhaa ya ushirikiano wa kimaendeleo ili Ukraine ijiunge na umoja huo.

Upande wa Ukraine ambao unapakana na Romania, Hungary, Slovakia na Poland, ambazo ni wanachama, huku Belarus na Moldoa zikiwa pia zimepakana ingawa sio nchiwanachama za Umoja wa Ulaya. Wananchi wengi wa upande huu wanazungumza Ki-Ukraine na wanaunga mkono kujiunga EU. Kla wa upande ambao wamepakana na Urusi, huzungumza lugha hiyo, na hawapendelei kujiunga na EU. Kilichofuatia, ni maandamano yasiyo na kikomo, na matukio ya kila aina;
Waandamanaji wanaoipinga serikali wakiwa Kiev Square, katikati ya mji wa Kiev, ambapo kwa sasa wamemshinikiza Rais Viktor Yanukovych ajiuzulu kutokana na kushindwa kuliongoza taifa ikiwemo tuhuma za rushwa na kutozingatia utawala bora. ©AP
Penye wengi kuna vijambo, mmojawapo wa waandamanaji alitumia fursa hii kumuomba mchumga wake wafunge ndoa, na sehemu pekee iliyompendeza kumvalishia pete ni eneo lenye machafuko. Pembeni yake wapambe ambao wamevaa mavazi mithili ya wanaeshi wakishuhudia tukio hilo la kihistoria. Bibie alikubali. ©AP

Habari  kwa hisani ya Gospel Kitaa
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment