Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, February 26, 2014

Uzembe wa jeshi waudhi wakaazi Nigeria


Ibrahim Geidam gavana wa jimbo la Yobe,Nigeria
Wakaazi wa mji mmoja kaskazini mashariki mwa Nigeria wameonyesha hasira dhidi ya majeshi ya usalama kwa kuondoa vituo vya ukaguzi kabla ya shambulio la wapiganaji wa Kiislam katika shule shule moja katika eneo hilo.
Vijana wapatao 29 waliuawa katika shambulio hilo, ambapo kikundi cha Boko Haram kimeshtumiwa kuishambulia shulehiyo iliyopo jimbo la Yobe.
Kituo kingine nje ya mji wa Buni Yadi pia walinzi wake waliondolewa wiki moja iliyopita.Wakaazi wanasema askari waliokuwa wakilinda katika kituo jirani cha ukaguzi, waliondolewa katika hali isiyotarajiwa kabla ya shambulio hilo.
Wanamgambo hao wa Kiislam waliishambulia shule hiyo usiku wa Jumatatu wiki hii.
Gavana wa jimbo la Yobe, Ibrahim Gaidam pia ameyashutumu majeshi ya usalama kwa ugoigoi mkubwa ulionyeshwa katika kukabiliana na tukio hilo, akisema saa tano zilipita bila ya askari wa usalama kuwasili katika eneo la tukio ili kuzima mauaji hayo.

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment