Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, February 5, 2014

17 wakwama mgodini Afrika Kusini

Wachimba migodi wamekuwa wakigoma wakilalamikia malipo duni
Vikosi vya uokozi vimeingia katika mgodi wa dhahabu nchini Afrika Kusini kujaribu kuwaokoa wafanyakazi 17 wa kuchimba mgodi waliokwama mgodini baada ya moto kuzuka.
Kampuni hiyo ya madini Harmony Gold,inasema kuwa moshi uliofuka pomoja na mawe yaliyokuwa yanaanguka yanasemekana kutatiza shughuli ya uokozi.
Kampuni hiyo inasema kuwa imeweza kuwasiliana na wachimba migodi walionaswa.
Kadhalika imesema kuwa imeweza kuwasiliana na wafanyakazi wengine 8 walioweza kujiokoa kutokana na moto uliozuka Jumanne usiku na kutafuta hifadhi katika kituo kimoja kilicho umbali wa mita 1700 chini ya ardhi .
Wachimba migodi tisa bado hawajulikani waliko.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment