Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, January 4, 2014

WAPENTEKOSTE TANZANIA KUFUNGA SIKU 40 KUANZIA JANUARI 6

Katibu mkuu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste nchini (PCT), Askofu Dkt. David Mwasota
Baraza la makanisa ya Kipentekoste limetangaza siku 40 za maombi kuanzia Januari 6, ambapo pamoja na kuombea amani, mengi pia yatawekwa mikononi mwa BWANA. Akiongea na wanahabari jijini Dar siku ya Ijumaa, katibu mkuu wa baraza la makanisa ya Kipentekoste, Askofu Dakta David Mwasota ananukuliwa akisema kuwa pamoja na kuliombea taifa amani, pia wataombea uchumi, gesi asilia na wizara inayohusika na gesi (Nishati na Madini), Wizara ya Maliasili na Utalii, TRA (Mamlaka ya mapato nchini), na Ardhi kwani wanaamini kuwa wizara zinazohusika na mambo hayo ndio zimeshikilia uchumi wa taifa.

sisi wapt tunaamini huo nduo uchumi wenyewe hizi nyingine zina mchango lakini hizi ndo zaidi
Pamoja na hayo, Askofu Mwasota amesema kuwa wayakuwa pia na jukumu la kuombea uchaguzi wa serikali za mitaa, pamoja na wa wabunge na rais 2015.

Halikadhalika mchakato wa katiba unaoendelea ni sehemu ya maombi ambayo PCT watafanya, ili kwamba mpango wa Mungu uweze kutimia, na wale wote wenye hila kuelekea kwenye Bunge Maalumu la Katiba wakashindwe kwa jina la Mungu.
Pia Ask Mwasota, ametoa pongezi kwa Rais Kikwete kwa hatua za utawala anazoshukua sasa hivi kwani zitarudisha nidhanu serikalini, na pia wanamuombea ili aweze kuteua baraza zuri la mawaziri.

Katika hatua nyingine pia PCT wametoa pongezi kwa Inspekta Jenerali wa Polisi mpya, Ernest Mangu, na kuahidi kutoa ushirikiano kama ambavyo wamekuwa wanatoa kupita kampeni mbalimbali ikiwemo ya kutii sheria bila shuruti, na ile ya Familia yangu haina mualifu.

Julai Mosi 2013, PCT ilikuwa na ratiba ya kufunga na kuomba kwa ajili ya taifa, ambapo takribani kwa siku 42 ratiba ilidumu na kudhihirisha nguvu ya Mungu kwa njia tofauti tofauti kwa taifa.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment